Kikosi cha majini cha IRGC ya Iran kuzindua nyambizi mpya za kisasa
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i50677-kikosi_cha_majini_cha_irgc_ya_iran_kuzindua_nyambizi_mpya_za_kisasa
Kamanda wa Kikosi cha Majini cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (SEPAH) amesema kikosi hicho kinatengeneza nyambizi za kisasa, na mafanikio hayo mapya ya Iran katika uga wa kujihami yatazinduliwa karibuni hivi.
(last modified 2026-03-17T04:36:21+00:00 )
Jan 06, 2019 04:41 UTC
  • Kikosi cha majini cha IRGC ya Iran kuzindua nyambizi mpya za kisasa

Kamanda wa Kikosi cha Majini cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (SEPAH) amesema kikosi hicho kinatengeneza nyambizi za kisasa, na mafanikio hayo mapya ya Iran katika uga wa kujihami yatazinduliwa karibuni hivi.

Katika mahojiano na shirika la habari la Tasnim, Admeri Ali Reza Tangsiri amesema kuimarisha uzalishaji wa nyambizi ni mojawapo ya mahitaji muhimu ya kuimarisha uwezo wa kiulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. 

Kamanda huyo wa IRGC amesema hivi sasa sekta ya ulinzi ya Iran ina uwezo wa kuandaa na kutengeneza kwa wingi nyambizi za kisasa kabisa.

Nyambizi ya Qadir ya Iran ya Kiislamu

Ameashiria mafanikio ya hivi karibuni ya kutengeneza nyambizi za kisasa kama vile Faatih, Qadir na Be'that, na kubainisha kuwa wataalamu wa jeshi la wanamaji la Iran sasa wako katika njia ya kufikia maendeleo na ustawi mkubwa zaidi katika uwanja huo.

Vikosi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran vimekuwa vikisisitiza kuwa, uwezo wake mkubwa kijeshi ni kudhihirisha uwezo wa kujilinda na chokochoko za maadui sambamba na kutuma ujumbe wa amani na urafiki kwa nchi za eneo hili kuwa vikosi hivyo vina uwezo wa kukabiliana na uvamizi wa maadui.