Kamanda: Jeshi la Iran liko tayari kutoa jibu kwa tishio lolote
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i50806-kamanda_jeshi_la_iran_liko_tayari_kutoa_jibu_kwa_tishio_lolote
Kamanda wa Jeshi la Anga la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema taifa hili limejiandaa kutoa jibu mwafaka kwa tishio lolote ajinabi.
(last modified 2026-08-03T07:36:50+00:00 )
Jan 11, 2019 23:24 UTC
  • Kamanda: Jeshi la Iran liko tayari kutoa jibu kwa tishio lolote

Kamanda wa Jeshi la Anga la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema taifa hili limejiandaa kutoa jibu mwafaka kwa tishio lolote ajinabi.

Brigedia Jenerali Aziz Nasirzadeh alisema hayo jana Ijumaa, pambizoni mwa luteka ya kijeshi iliyofanyika katika mkoa wa Isfahan, katikati mwa Iran.

Amesema "Ujumbe wetu kwa taifa la Iran, ni kwamba tuko tayari kujibu vitisho vyovyote."

Kadhalika amesema mazoezi hayo ya kijeshi yanatuma ujumbe wa urafiki na amani kwa nchi za eneo, na kuzitanabaisha kuwa, "Kadri usalama wa eneo unavyoimarika, ndivyo tunavyozidi kuonesha kuwa hatuhitaji uwepo wa maajinabi katika eneo."

Maneva ya kijeshi ya Fadayeeyan Harim Velayat 8 mjini Isfahan

Katika siku ya pili ya maneva hayo ya kijeshi yaliyopewa jina "Walinzi wa Kujitolea wa Velayat 2019", ndege za kijeshi za Iran za F-4 Phantom zililenga kwa ustadi 'adui' kwa kudondosha makombora ya angani hadi ardhini ya 'Maverick' na mabomu-erevu ya 'Qassed' yaliyotengenezwa na wataalamu wa hapa nchini.

Maneva hayo yaliyofanyika Isfahan yalishuhudia Jeshi la Anga la Iran likionesha ustadi wa ndege za kivita za kudondosha mabomu ya Sukhoi Su-24, F-4, F-5, F-7, MiG-29, F-14, Boeing 707 na 747 pamoja na ndege maalumu inayotumika kujaza mafuta kwenye ndege za kijeshi ya C130.

Kadhalika ndege za kisasa zisizo na rubani (drones) zilitumika katika mazoezi hayo ya kijeshi yaliyoanza Alkhamisi.