Iran: Marekani inawahamishia magaidi wa DAESH (ISIS) Afghanistan
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i51355-iran_marekani_inawahamishia_magaidi_wa_daesh_(isis)_afghanistan
Msaidizi na Mshauri Mwandamizi wa Amiri Jeshi Mkuu wa vikosi vya ulinzi vya Iran amesema: Jamhuri ya Kiislamu ina taarifa za uhakika kuhusu hatua inazochukua Marekani za kuwahamishia magaidi wa kundi la ukufurishaji la DAESH (ISIS) nchini Afghanistan.
(last modified 2026-03-03T12:46:59+00:00 )
Feb 05, 2019 12:29 UTC
  • Iran: Marekani inawahamishia magaidi wa DAESH (ISIS) Afghanistan

Msaidizi na Mshauri Mwandamizi wa Amiri Jeshi Mkuu wa vikosi vya ulinzi vya Iran amesema: Jamhuri ya Kiislamu ina taarifa za uhakika kuhusu hatua inazochukua Marekani za kuwahamishia magaidi wa kundi la ukufurishaji la DAESH (ISIS) nchini Afghanistan.

Meja Jenerali Sayyed Yahya Rahim Safavi ameyasema hayo leo katika hafla maalumu ya maadhimisho ya mwaka wa 40 wa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu iliyofanyika hapa mjini Tehran, ambapo sambamba na kuashiria kushindwa Marekani katika nchi za Iraq na Afghanistan ameongeza kuwa: Nguvu za Marekani na Wazayuni zinafifia.

Meja Jenerali Safavi ameashiria matunda na mafanikio iliyopata Iran katika miaka 40 iliyopita na kubainisha kwamba: Katika miaka 40 iliyopita, Iran imegeuka kuwa dola kuu la kieneo kwa kuongeza nguvu na uwezo wake wa kiulinzi kwa ajili ya kukabiliana na Wazayuni; na kutokana na hatua hiyo Mapinduzi ya Kiislamu yanaweza kuwa ruwaza na mfano wa kuigwa na Waislamu na wapigania ukombozi duniani.

Msaidizi na Mshauri Mwandamizi wa Amiri Jeshi Mkuu wa vikosi vya ulinzi vya Iran amezungumzia tadbiri na uono wa mbali wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika kadhia ya Syria na kueleza kwamba: Kutokana na njama ya Wamarekani, Wazayuni na baadhi ya nchi za Kiarabu, magaidi zaidi laki moja wa kundi la kitakfiri la Daesh walizishambulia na kuzivamia kijeshi Syria na Iraq, hata hivyo Iran iliweza kuzima njama za maadui hao kwa hatua ilizochukua baada ya kuombwa msaada na nchi hizo mbili.../