Ayatullah Khatami: Madola ya Kiistikbari hayalitakii kheri taifa la Iran
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i51418-ayatullah_khatami_madola_ya_kiistikbari_hayalitakii_kheri_taifa_la_iran
Khatibu wa Swala ya Ijumaa iliyoswaliwa leo hapa mjini Tehran amesema kuwa, madola ya kiistikbari hayalitakii kheri taifa la Iran, hivyo maafisa wa serikali hawapaswi kuwa na matumaini na madola hayo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 08, 2019 10:42 UTC
  • Ayatullah Khatami: Madola ya Kiistikbari hayalitakii kheri taifa la Iran

Khatibu wa Swala ya Ijumaa iliyoswaliwa leo hapa mjini Tehran amesema kuwa, madola ya kiistikbari hayalitakii kheri taifa la Iran, hivyo maafisa wa serikali hawapaswi kuwa na matumaini na madola hayo.

Ayatullah Sayyid Ahmad Khatami amesema hayo leo mbele ya hadhara kubwa ya waumini waliohudhuria ibada ya kimaanawi na kisiasa ya Swala ya Ijumaa mjini Tehran ambapo ameashiria kuchelewa kwa muda mrefu utekelezwaji wa mkakati wa mfumo wa kifedha baina ya Iran na madola ya Ulaya na masharti ya madola hayo kwa ajili ya kulindwa na kuhifadhiwa makubaliano ya nyuklia ya JCPOA kwa kuliunganishwa hilo na masuala kama ya Shirikisho la Kupambana na Fedha Chafu na Ufadhili wa Makundi ya Kigaidi (FATF) na mazungumzo kuhusu mpango wa makombora wa Iran na kueleza kuwa, kujiunga au kutojiunga Iran na taasisi ya FATF ni uamuzi wa ndani ya mfumo.

Khatibu wa Swala ya Ijumaa mjini Tehran amesema kuwa, kusimama kidete kwa wananchi wa Iran kutalifanya taifa hili livuke salama pia kipindi hiki cha vikwazo vya kidhalimu.

Swala ya Ijumaa mjini Tehran-08.02.2019

Ayatullah Ahmad Khatami aidha amesema bayana kwamba, matatizo ya sasa ya Iran yatapatiwa ufumbuzi kwa usimamizi wa kijihadi na kwa kuwachukulia hatua kali mafisadi.

Khatibu wa muda wa Swala ya Ijumaa mjini Tehran ameashiria pia kuonyeshwa kombora la balestiki la Dezful lenye uwezo wa kwenda masafa ya kilomita elfu moja na kusema kuwa, kombora hilo limezinduliwa katika fremu ya kuendelezwa siasa za kujilinda na za kiulinzi za mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu.

Ayatullah Khatami amewataka pia wananchi wa Iran kujitokeza kwa wingi katika maandamano ya maadhimisho ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu Jumatatu ijayo.