Dakta Zarif: Daima Iran imekuwa ikifuatilia suala la kuisaidia Afghanistan
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i52212-dakta_zarif_daima_iran_imekuwa_ikifuatilia_suala_la_kuisaidia_afghanistan
Dakta Muhammad Javad Zarif, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, daima Iran imekuwa ikifuatilia suala la kuisaidia serikali na wananchi wa Afghanistan.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 17, 2019 02:23 UTC
  • Dakta Zarif: Daima Iran imekuwa ikifuatilia suala la kuisaidia Afghanistan

Dakta Muhammad Javad Zarif, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, daima Iran imekuwa ikifuatilia suala la kuisaidia serikali na wananchi wa Afghanistan.

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema hayo katika mazungumzo yake hapa mjini Tehran na Mohammad Omar Daudzai mwakilishi wa Rais wa Afghanistan katika masuala ya amani na kusisitiza kwamba, serikali ya Kabul ndio mwakilishi wa wananchi wa Afghanistan hivyo inapaswa kutangaza msimamo wake katika masuala yote.

Dakta Zarif amesisitiza kwamba, siku zote Iran imekuwa pamoja na serikali na wananchi wa Afghanistan na daima imekuwa ikifuatilia suala la kulisaidia taifa hilo.

Kwa upande wake Mohammad Omar Daudzai mwakilishi wa Rais wa Afghanistan katika masuala ya amani amepongeza misimamo chanya  ya Iran na jinsi Tehran inavyoonyesha kuguswa na masuala yanayoihusu Kabul.

Rais Ashraf Ghani wa Afghanistan

Katika mazungumzo hayo, pande mbili mbali na kujadili masuala ya kieneo, Mohammad Omar Daudzai mwakilishi wa Rais wa Afghanistan katika masuala ya amani amebainisha kwa kina kuhusu matukio ya hivi karibuni kabisa katika nchi yake.

Dakta Muhammad Javad Zarif, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amebadilisha mawazo pia na Mohammad Omar Daudzai mwakilishi wa Rais wa Afghanistan katika masuala ya amani kuhusiana na njia za kustawishwa uhusiano na ushirikiano baina ya Tehran na Kabul.

Mohammad Omar Daudzai mwakilishi wa Rais wa Afghanistan katika masuala ya amani aliwasili jana Jumamosi hapa mjini Tehran kwa shabaha ya kukutana na kufanya mazungumzo na viongozi mbalimbali hapa nchini.