Tehran mwenyeji wa Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa India
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i58036-tehran_mwenyeji_wa_waziri_wa_mashauri_ya_kigeni_wa_india
Hivi karibuni Tehran ilikuwa mwenyeji wa mkutano wa Makatibu wa Mabaraza Makuu ya Usalama na viongozi wa usalama wa baadhi ya nchi jirani na Afghanistan.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 22, 2019 04:42 UTC
  • Tehran mwenyeji wa Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa India

Hivi karibuni Tehran ilikuwa mwenyeji wa mkutano wa Makatibu wa Mabaraza Makuu ya Usalama na viongozi wa usalama wa baadhi ya nchi jirani na Afghanistan.

Leo Jumapili Tehran ni mwenyeji wa Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa India. Katika fremu ya safari hiyo, kutafanyika kikao cha 19 cha kamisheni ya pamoja ya Iran na India kitakachoongozwa na Muhammad Javad Zarif, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran na Subrahmanyam Jaishankar, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa India.

Kabla ya hapo pia, Mawaziri wa Mashauri yya Kigeni wa India na Iran wamewahi kufanya vikao vya pamoja kuhusianan na masuala ya nishati, matukio ya Afghanistan na ushirikiano wa pande kadhaa wa kieneo. Safari ya Subrahmanyam Jaishankar, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa India inapaswa kutathminiwa pia katika fremu ya uhuusiano wa pande mbili na ushirikiano wa kisiasa na kiuchumi wa Tehran na New Delhi.

India ni moja ya nchi kubwa kwa matumizi ya nishati katika uga wa kimataifa. Hivyo basi ni jambo la kawaida kwamba, hatua yoyote ile ya kuitatiza nchi hiyo kupata nishati hiyo, kunaweza kuwa na taathira hasi kwa uchumi wa nchi hiyo. Ni kutokana na sababu hiyo ndio maana India inazingatia mno suala la kulinda na kustawisha uhusiano wake wa kiuchumi na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Bendera za Iran na India

Ni kwa muktadha huo ndio maana kipengee cha tatu cha taarifa ya mwisho ya kikao cha pili cha Makatibu wa Mabaraza Makuu ya Usalama wa Taifa na maafisa wa ngazi za juu wa usalama wa nchi za eneo ikiwemo India sanjari na kuashiria umuhimu wa nishati katika kukuza na kustawisha uchumi wa nchi za eneo na ulimwengu kwa ujumla, kinasisitiza haki ya nchi zote zinazouza mafuta na nishati kudhamini mahitaji ya soko la nishati na haki ya nchi zinazonunua kuwa na uhuru kamili wa kulifikia soko la nishati.

Kwa kuuzingatia yote hayo, safari ya Waziri wa Mashauri ya Kigeni hapa mjini Tehran  kwa upande mmoja inapaswa kutathminiwa kama lengo lake ni kuimarisha uhusiano unaokua baina ya Tehran na New Delhi; na katika upande mwingine ina umuhimu wa kidiplomasia hasa kwa kuzingatia matukio ya eneo.

Vahid Dindari mtaalamu na mweledi wa masuala ya kisiasa anasema: Viongozi wa India wanafahamu vyema kwamba, maslahi ya nchi hiyo yamo katika uhusiano wa nchi hiyo na Iran ukiwemo uga wa kudhamini nishati ambapo haiwezekani kulifumbia macho jambo hilo.

Rais Hassan Rouhani akiwa na Narendra Modi, Waziri Mkuu wa India

Kwa hakika safari ya Subrahmanyam Jaishankar, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa India hapa Tehran inafanyika katika kipindi ambacho nchi mbili hizo zimefikia makubaliano ya kupanua ushirikkiano wa kibiashara baina yao na zinakusudia kuandaa mikakati zaidi kwa ajili ya ushirikiano huo.

Surajit Air, mchambuzi wa masuala ya kiuchumi anaashiria umuhimu wa Iran kwa India katika kufanyika mabadilishano ya kibiashara na uingizaji wa nishati na kubainisha kwamba:

Endapo washirika wa India kama Marekani watalalamikia uhusiano mzuri wa Tehran na New Delhi, basi India inapaswa kuwa na msimamo imara na isisalimu amri mbele ya matakwa yao. Hapana shaka kuwa, India itanufaika kwa kuchukua msimamo kama huu, kinyume na hivyo itakuwa mhanga wa siasa zinazobadilika za washiriak wake na madola makubwa ya dunia hususan Marekani. Iwapo India itashindwa kufanya hilo, basi itakuwa imepoteza fursa ya dhahabu.

Subrahmanyam Jaishankar, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa India

Mazungumzo haya na safari za pande mbili zinafanyika katika hali ambayo, Marekani imeshadidisha mashinikizo yake dhidi ya waitifaki wake wa Ulaya na Asia, ili kwa njia hiyo kama inavyodai iweze kuitenga Iran. Pamoja na hayo, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeendelea kuwa na nafasi amilifu na athirifu kwa matukio ya eneo. Katika uwanja huo, Juzi, baada ya kushiriki katika mkutano wa Kuala Lumpur 2019, Rais Hassan Rouhani wa Iran alifanya safari nchini Japan.

Mtazamo wa Iran ni kupanua ushirikiano na nchi za mashariki mwa Asia, na ndio maana hilo limekuwa ajenda kuu katika mazungumzo na safari hizi. Hapana shaka kuwa, India nayo ina hisa kubwa katika mchakato huu. Kwa mtazamo huu, mazungumzo ya Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa India hapa mjini Tehran na kufanyika kikao cha kamisheni ya pamoja ya nchi mbili inapaswa kutambuliwa kama ni ishara ya azma na irada ya Tehran na New Delhi ya kuimarisha ushirikiano baina yao.