Namaki: Hali ya wagonjwa wa COVID-19 Iran inaboreka
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i64912-namaki_hali_ya_wagonjwa_wa_covid_19_iran_inaboreka
Waziri wa Afya wa Iran amesema hali ya wagonjwa wa COVID-19 au corona nchini Iran inaboreka.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 29, 2020 08:42 UTC
  • Namaki: Hali ya wagonjwa wa COVID-19 Iran inaboreka

Waziri wa Afya wa Iran amesema hali ya wagonjwa wa COVID-19 au corona nchini Iran inaboreka.

Akizungumza leo Jumapili katika Kikao cha Hatua ya Nne ya Mshikamano wa Kitaifa katika Kukabiliana na COVID-19 ambayo imepewa jina la 'Mpango wa Shahidi Qassem Soleimani', Daktari Saeed Namaki amesema: "Hali ya wagonjwa wa corona nchini hasa katika miji midogo imeanza kuboreka kufuatia vizuio vilivyotekelezwa"

Namaki ameashiria baadhi ya watu waliotabiri kuwa vifo kutokana na corona vitafika 800 hadi 1000 kwa siku nchini Iran na kusema: "Kwa bahati nzuri hali imenza kuboreka nchini na bado matokeo kamili ya mpango wa 'Shahidi Qassem Soleimani' hayajadhihirika"

Waziri wa Afya amesema serikali imeazimia kuongeza idadi vya vituo vya kupima corona hadi elfu tano ili watu wanaoshukiwa kuwa na corona waweze kupimwa haraka.

Aidha amesema Hatua ya Nne ya Mshikamano wa Kitaifa katika Kukabiliana na COVID-19 pia inajumuisha kuwasaidia wasiojiweza katika jamii waweze kukidhi mahitaji yao ya kimsingi na ya kila siku ili kwa njia hiyo ugonjwa wa corona uangamizwe kikamilifu.

Kwa mujibu wa takwimu za Wizara ya Afya walioambukizwa corona nchini Iran hadi sasa ni zaidi ya 935,000 na miongoni mwao zaidi ya watu 650,000 wamepona.