Kiongozi Muadhamu: Kisasi dhidi ya wauaji wa Qassim Suleimani hakina shaka
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i65231-kiongozi_muadhamu_kisasi_dhidi_ya_wauaji_wa_qassim_suleimani_hakina_shaka
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, wauaji wa Luteni Jenerali Qassim Suleimani lazima walipiziwe kisasi na kisasi hiki hakina shaka na kitatekelezwa wakati wowote.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 16, 2020 07:57 UTC
  • Kiongozi Muadhamu: Kisasi dhidi ya wauaji wa Qassim Suleimani hakina shaka

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, wauaji wa Luteni Jenerali Qassim Suleimani lazima walipiziwe kisasi na kisasi hiki hakina shaka na kitatekelezwa wakati wowote.

Ayatullah Ali Khamenei amesema hayo leo alipokutana na wajumbe wa Kamati ya Hauli ya Luteni Jenerali Qassim Suleimani aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (SEPAH) pamoja na familia ya shahidi huyo na kueleza kwamba, Shahidi Suleimani ni shujaa wa taifa la Iran na Umma wa Kiislamu.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa, kwa kuzingatia kwamba, Shahidi Qassim Suleimani alikuwa mtu wa watu ili kufanya kumbukumbu na hauli yake pia kuna haja ya kutumiwa uwezo wa wananchi na juhudi za kiutamaduni zenye ubunifu.

Luteni Jenerali Qassim Suleimani aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (SEPAH)

 

Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema kuwa, kuuawa Shahidi Luteni Jenerali Qssim Suleimani lilikuwa tukio chungu la kihistoria ambapo sambamba na kuashiria kubadilishwa shahidi huyo na kuwa shujaa wa taifa kwa ajili ya Wairani na shujaa wa Umma wa Kiislamu amesema kuwa, shahidi huyo mwenye daraja kubwa alikuwa mtu wa kimaanawi, ikhlasi na wa akhera na hakuna wakati ambao alikuwa akifanya mambo kwa kujionyesha.

Kadhalika Ayatullah Khamenei sanjari na kusema kuwa, Shahidi Qassim Suleimani aliushinda Ustikbari katika kipindi cha uhai wake na hata baada ya kuuawa kwake shahidi ameongeza kuwa, shughuli ya kusindikiza miili ya mashahidi Qassim Suleimani na Abu Mahdi al-Muhandis iliyohudhuriwa na mamilioni ya watu nchini Iran na Iraq iliwashangaza majenerali wa vita baridi vya Uistikbari na hicho kikawa kibao cha kwanza cha uso dhidi ya Wamarekani.