Amir-Abdollahian: Muqawama wa Yemen umewafadhaisha na kuwakanganya watawala wa Saudia
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i68210-amir_abdollahian_muqawama_wa_yemen_umewafadhaisha_na_kuwakanganya_watawala_wa_saudia
Hossein Amir-Abdollahian, mshauri maalumu wa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika masuala ya kimataifa amesema, leo baada ya miaka sita ya uvamizi uliofanywa kwa ushirikiano wa Marekani na Saudi Arabia, muqawama wa Yemen umeibuka mshindi na watawala wa Saudia wamefadhaika na kuchanganyikiwa.
(last modified 2026-08-12T14:02:06+00:00 )
Mar 23, 2021 03:41 UTC
  • Amir-Abdollahian: Muqawama wa Yemen umewafadhaisha na kuwakanganya watawala wa Saudia

Hossein Amir-Abdollahian, mshauri maalumu wa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika masuala ya kimataifa amesema, leo baada ya miaka sita ya uvamizi uliofanywa kwa ushirikiano wa Marekani na Saudi Arabia, muqawama wa Yemen umeibuka mshindi na watawala wa Saudia wamefadhaika na kuchanganyikiwa.

Katika ujumbe alioandika kwenye ukurasa wake wa kijamii wa twitter, Amir-Abdollahian amesema, miaka sita imepita ya muqawama wa watu wa Yemen wa kukabiliana na uvamizi wa pamoja wa Marekani na Saudia.

Mshauri maalumu wa Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran katika masuala ya kimataifa ameongeza kuwa, waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Saudia Adel al Jubeir alikuwa amedai kwamba "tutawaangamiza Mahouthi kwa siku 15".

Katika ujumbe wake huo, Amir-Abdollahian amesisitiza kuwa, vita sio njia ya utatuzi, njia ya utatuzi wa kadhia ya Yemen ni ya kisiasa tu.

Mshauri maalumu wa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika masuala ya kimataifa amebainisha kuwa, leo muqawama wa Yemen umeshinda na watawala wa Aal Saudi wamefadhaika na kuchanganyikiwa mno.../