Rais Rouhani: Hakuna kizuizi cha kupanuliwa ushirikiano baina ya Iran na Qatar
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i72546-rais_rouhani_hakuna_kizuizi_cha_kupanuliwa_ushirikiano_baina_ya_iran_na_qatar
Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Iran na Qatar zikiwa nchi mbili za Kiislamu zina uhusiano mzuri.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 19, 2021 10:57 UTC
  • Rais Rouhani: Hakuna kizuizi cha kupanuliwa ushirikiano baina ya Iran na Qatar

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Iran na Qatar zikiwa nchi mbili za Kiislamu zina uhusiano mzuri.

Rais Rouhani amesema hayo katika mazungumzo yake kwa njia ya simu na Amir wa Qatar Tamim bin Hamad Al Thani ambapo sambamba na kuashiria dursa nyingi zilizopo kwaajili ya ushirikiano katika nyanja zote amebainisha kwamba, hakuna kizuizi cha kupanuliwa ushirikiano baina ya nchi mbili hizi.

Rais Rouhani amesema pia kuwa, mazingira ya sasa yanayotawala katika eneo la Asia Magharibi na ulimwengu kwa ujuma yanalazimu kuweko ushirikiano na mawasiliano ya kuendelea baina ya Doha na Tehran.

Kadhalika Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema, kufanya juhudi kwa ajili ya kupatikana amani na usalama katika eneo ni miongoni mwa sera kuu ambao zimekuwa zikifuatiliwa na serikali ya Tehran.

Bendera za Iran na Qatar

 

Dakta Rouhani ameipongeza Qatar kutokana na misimamo yake thabiti kuhusiana na masuala mbalimbali ya eneo na kusisitizia ulazima wa kufanyika mazungumzo kwa ajili ya kuipatia ufumbuzi migogoro iliyopo kwa njia za amani.\

Kwa upande wake Amir wa Qatar Tamim bin Hamad Al Thani amesema kuwa, uhusiano wa nchi mbili ni wa kirafili na upo katika hatua nzuri mno na akasisitiza kwamba, Doha inaamini kwamba, mizozo ya eneo hili haiwezi kupatiwa ufumbuzi kwa mtutu wa bunduki; bali mazungumzo ndio njia bora kabisa ya kuipatia ufumbuzi mizozo hiyo.