Msimamo wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu kuhusu kudhalilishwa Marekani huko Afghanistan
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i72594-msimamo_wa_kiongozi_wa_mapinduzi_ya_kiislamu_kuhusu_kudhalilishwa_marekani_huko_afghanistan
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei amesema ufahamu usio sahihi wa Marekani meifanya idhalilishwe nchini Afghanistan.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 21, 2021 02:47 UTC
  • Msimamo wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu kuhusu kudhalilishwa Marekani huko Afghanistan

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei amesema ufahamu usio sahihi wa Marekani meifanya idhalilishwe nchini Afghanistan.

Ayatullah Khamenei ameyasema hayo katika ujumbe wake wa Hija ya mwaka huu ambako aliashiria ahadi ya kweli ya Mwenyezi Mungu ya kuwapa nusra na ushindi wapiganaji wa Jihadi na kusema:  Athari ya kwanza ya Jihadi hiyo ni kuizuia Marekani na madola mengine ya kibeberu kuingilia na kufanya vitendo vya shari katika nchi za Waislamu. Amezungumzia jinai zilizofanywa na Marekani huko Afghanistan katika kipindi cha miaka 20 iliyopita na kusema: Ufahamu usio sahihi wa serikali ya Washington ndio ulioifanya Marekani idhalilishwe nchini Aghanistan. 

Kuhusu matokeo ya ufahamu huo usio sahihi wa viongozi wa White House huko Afghanistan, Ayatullah Khamenei amesema: Baada ya kutumia silaha, mabomu na zana nyingine za vita dhidi ya watu na raia wasio na hatia wa Afghanistan, Marekani imejipata katika kinamasi na kulazimika kuondoa majeshi na zana zake za kivita katika nchi hiyo. 

Akiashiria mwendelezo wa njama chafu za Marekani dhidi ya nchi za Mashariki mwa Asia, Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema: "Taifa lenye mwamko la Afghanistan linapasa kuwa macho kuhusiana na vyombo vya ujausi na silaha za vita laini za Marekani katika ardhi ya nchi hiyo. Taifa hilo lipasa kusimama imara mbele ya vyombo na silaha hizo." 

Ayatullah Khamenei: Taifa la Afghanistan linapasa kuwa macho kuhusiana na vyombo vya ujausi na silaha za vita laini za Marekani.

Japokuwa Marekani imeamua kuyaondoa majeshi yake vamizi huko Afghanistan baada ya kutumbukia katika kinamasi kikubwa kilichosababishwa na utendaji usio sahihi, lakini inatupasa kusisitiza tena kwamba, kuondoka huko hakuna maana ya kumalizika kazi na njama za Washington nchini Afghanistan. Hii ni kwa sababu, Washington inafanya jitihada za kuendeleza uwepo wake wa kijasusi na kiupelelezi katika nchi hiyo kwa shabaha ya kudumisha sera na mipango yake inayokinzana na maslahi ya nchi za kanda hii ya Asia. 

Kwa msingi huo mbali na kukabiliwa na vita na hujuma za kiupelelezi na kijasusi ya Marekani, Aghanistan inawajihiana pia na silaha za vita laini za White House. Ni kwa kutilia maanani mazingira haya ndipo Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu akawataka watu wa Afghanistan kuwa macho mbele ya zana za kijasusi na silaha za vita laini za Marekani, na kukabiliana nazo kwa umakini mkubwa.

Katika kipindi cha miaka 20 iliyopita Marekani haikutimiza ahadi zake za kukabiliana na kukomesha ugaidi nchini Afghanistan na kinyume chake, imewaua maelfu ya raia wasio na hatia wa nchi hiyo katika mashambulizi yake ya anga na nchi kavu kutokana na tabia yake ya kujichukulia maamuzi ya upande mmoja na yasiyo sahihi. Ni kwa sababu hiyo pia ndiyo maana mashirika ya kimataifa ya kutetea haki za binadamu yametoa wito wa kushughulikiwa jinai za kivita na dhidi ya binadamu zilizofanywa na majeshi ya Marekani huko Afghanistan.     

Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) Fatou Bensouda anasema: Taarifa zinaonesha kuwa majeshi ya Marekani yamefanya jinai za mateso, mienendo ya kikatili, kuwadhalilisha raia, ubakaji na unyama dhidi ya wafungwa nchini Afghanistan hususan katika kipindi cha kati ya mwaka 2003 na 2004. 

Fatou Bensouda

Kwa sasa Marekani inafanya jitihada za kukimbia kinamasi cha Afghanistan baada ya kushindwa na kufeli sera za siasa zake nchini humo lakini ukweli ni kwamba, uamuzi huo ni mwanzo wa kuwepo katika sura mpya huko Aghanistan katika kalibu ya hujuma ya kijasusi na vita vya silaha laini ambavyo uharibifu wake ni mkubwa maradufu kuliko kuwepo kwa majeshi ya nchi hiyo katika ardhi ya Afghanistan.