Shamkhani: Mazungumzo ya Vienna hayatafanikiwa kama Washington haitaachana na njozi zake
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i80126-shamkhani_mazungumzo_ya_vienna_hayatafanikiwa_kama_washington_haitaachana_na_njozi_zake
Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran amesema kuwa mazungumzo ya Vienna hayatafanikiwa kama Washington haitaachana na njozi zake.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 08, 2022 09:11 UTC
  • Ali Shamkhani
    Ali Shamkhani

Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran amesema kuwa mazungumzo ya Vienna hayatafanikiwa kama Washington haitaachana na njozi zake.

Ali Shamkhani leo Jumanne ameandika katika ukurasa wake wa Twitter kabla kuanza duru ya nane ya mazungumzo kati ya Iran na kundi la 4+1 huko Vienna kwa ajili ya kuondoa vikwazo vya Marekani dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu kwamba: Serikali ya sasa ya Marekani imeendeleza sera za mashinikizo ya kiwango cha juu za Trump dhidi ya Iran na kufanya jitihada za kufanikisha malengo yake iliyoshindwa kuyafikia kwa kutumia mabavu kupitia njia ya kutoa ahadi hewa.  

Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran ameashiria katika ukurasa wake wa Twitter kuwa: Bado kuna mpemgo kubwa hadi kupatikana mlingano unaohitajika kuhusiana na ahadi na vitendo vya pande husika katika mazungumzo ya Vienna na kwamba maamuzi yanayochukuliwa huko Washington yanahitajia mlingano katika kuwajibika ili kufikia mapatano mazuri.   

Wakati huohuo Ali Bagheri Kani kiongozi wa timu ya mazungumzo ya Iran leo asubuhi ameelekea mjini Vienna, Austria. Duru mpya ya mazungumzo ya Vienna ilisitishwa tarehe 28 mwezi Januari mwaka huu ili kutoa fursa kwa jumbe husika katika mazungumzo hayo kuendelea na mashauriano katika miji mikuu ya nchi zao na kuchukua maamuzi ya kisiasa yatakayofanikisha kufikiwa mapatano.  

Saeed Khatibzadeh Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran jana alitangaza kuwa Iran inataraji upande wa pili utachukua maamuzi muhimu na ya dharura hususan  Marekani. 

Saeed Khatibzadeh, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran