Vahidi: Iran itakabiliana ipasavyo na mrengo wa kitakfiri na kigaidi
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i82250-vahidi_iran_itakabiliana_ipasavyo_na_mrengo_wa_kitakfiri_na_kigaidi
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Iran amesema: "Watu wanaoendeleza fikra za kitakfiri na wahalifu waliotekeleza mauaji kwenye Haram ya mjukuu wa Mtume Muhammad (saw) katika mji wa Mash'had hapa nchini, watachukuliwa hatua kali.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 07, 2022 09:17 UTC
  • Vahidi: Iran itakabiliana ipasavyo na mrengo wa kitakfiri na kigaidi

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Iran amesema: "Watu wanaoendeleza fikra za kitakfiri na wahalifu waliotekeleza mauaji kwenye Haram ya mjukuu wa Mtume Muhammad (saw) katika mji wa Mash'had hapa nchini, watachukuliwa hatua kali.

Ni baada ya tukio la Jumanne jioni, wakati mwanachama mmoja wa makundi ya kitakfiri aliposhambulia na kuwadunga kisu wanazuoni watatu wa Kiislamu waliokuwa wamekwenda kuzuru kaburi la mjukuu wa Mtume Muhammad (saw), Imam Ali bin Musa al Ridha (as) na kumuua mmoja miongoni mwao.  Wanazuoni wenzake wawili wamejeruhiwa katika hujuma hiyo ya kigaidi. 

Gaidi aliyetekeleza hujuma hiyo alikamatwa na kukabidhiwa kwa maafisa wa upelelezi na usalama wa Iran.

Gaidi aliwashambulia wanazuoni watatu mjini Mash'had

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Jamhuri ya Kiislamu, Ahmad Vahidi amewaambia waandishi wa habari mapema leo Alkhamisi kwamba tukio hilo chungu la siku ya Jumanne katika Haram ya Imam Ridha (AS) linaonyesha kwamba adui haachi kuendeleza unafiki na kusema: "Ugaidi ni matokeo ya mtazamo wa kibeberi, na mabeberu ndio walioanzisha Daesh na makundi mengine ya kigaidi. 

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Iran amesema: "Hatua hii inaonyesha kwamba, wanazuoni wa Kiislamu siku zote wamekuwa mstari wa mbele katika kutoa huduma na pia wa kwanza katika kushambuliwa na kuhujumiwa na madui."

Vahidi ameongeza kuwa, adui anajaribu kutumia vibaya tofauti za kikaumu na kimadhehebu baina ya mataifa rafiki, jambo ambalo halitafanikiwa."

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Iran ameongeza kuwa: "Nchi za Magharibi hususan Marekani, kamwe haziwezi kulaani vitendo hivyo kwa sababu zinaunga mkono itikadi ya kigaidi ya kitakfiri.