Raisi: Iran haitaruhusu Israel kutishia usalama wa kieneo
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i82518-raisi_iran_haitaruhusu_israel_kutishia_usalama_wa_kieneo
Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema Iran inafuatilia kwa karibu harakati za utawala wa Israel katika eneo na haitaruhusu utawala huo utishie usalama wa eneo kupitia nchi yoyote.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 14, 2022 23:32 UTC
  • Raisi: Iran haitaruhusu Israel kutishia usalama wa kieneo

Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema Iran inafuatilia kwa karibu harakati za utawala wa Israel katika eneo na haitaruhusu utawala huo utishie usalama wa eneo kupitia nchi yoyote.

Raisi ametoa tamko hilo Alhamisi mjini Tehran wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iraq Fuad Hussein. Katika kikao hicho, Raisi alisisitiza kuhusu uhusiano wa karibu baina ya Iran na Iraq na kuongeza kuwa, hakuna adui anayweza kuibua mfarakano baina ya nchi hizo mbili.

Amesema Iran inataraji kuwa, nchi jirani hasa Iraq, hazitaruhusu maadui kutumia ardhi zao kutishia usalama wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Ameongeza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inafuatilia kwa karibu harakati za utawala wa Kizayuni wa Israel katika eneo na hivyo uhusiano na utawala huu unaoua watoto hauwezi kufichika.  Raisi ameendelea kubaini kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran daima imekuwa ikisisitiza umuhimu wa kuwepo mshikamano, na umoja baina ya makundi yote ya kikabila, kidini, na kimadhehebu nchini Iraq ili uthabiti udumu nchini humo.

Fuad Hussein

Kwingineko katika mazungumzo hayo, Rais wa Iran amesema magaidi wakufurishaji wa ISIS au Daesh waliibuliwa na tawala za Marekani na Israel na hivi sasa wanatekeleza maagizo ya tawala hizo mbili nchini Afghanistan.

Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Nje wa Iraq amesema kwa mtazamoa wa Baghdad, si tu kuwa Iran ni nchi jirani bali ni nchi muitifaki na rafiki.  Amesema Iraq katu haitaruhusu ardhi yake itumike dhidi ya Iran.