Kan'ani: Wazayuni hawana mamlaka ya kutoa maoni kuhusu haki za binadamu
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i91224-kan'ani_wazayuni_hawana_mamlaka_ya_kutoa_maoni_kuhusu_haki_za_binadamu
Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran mesema kuwa utawala wghasibu, wa kigaidi na wa kibaguzi wa Israel hauna mamlaka yoyote ya kimaadili ya kutoa maoni kuhusu suala la haki za binadamu.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 02, 2022 07:20 UTC
  • Kan'ani: Wazayuni hawana mamlaka ya kutoa maoni kuhusu haki za binadamu

Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran mesema kuwa utawala wghasibu, wa kigaidi na wa kibaguzi wa Israel hauna mamlaka yoyote ya kimaadili ya kutoa maoni kuhusu suala la haki za binadamu.

Haki za wananchi madhulumu wa Palestina zimekuwa zikikandamizwa na utawala ghasibu wa Israel kwa zaidi ya miaka sabini. Utawala huu umefanya jinai za kutisha na za kikatili zaidi dhidi ya Wapalestina katika kipindi chote cha uvamizi na kukaliwa kwa mabavu ardhi ya Palestina.

Kuhusiana na hilo na kwa mujibu wa shirika la habari la Mehr, Nasser Kan'ani Chafi, msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran, ameandika kwenye ukurasa wa Twitter kwamba: "Wanaofanya uhalifu dhidi ya mataifa mengine na waungaji mkono wa utawala ghasibu, wa kigaidi na wa kibaguzi wa Israel hawana mamlaka ya kimaadili ya kutoa maoni juu ya haki za binadamu na utendaji wa nchi nyingine katika uwanja huu."

Kan'ani Chafi ameongeza kuwa: Haki za binadamu ni dhana takatifu, na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inalitambua suala la kuboresha haki hizo kuwa ni dharura ya Kiislamu, kiutu, kisheria na kimaadili.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema: Wakiukaji wa haki za binadamu wanapaswa kuacha kutumia haki za binadamu kama wenzo wa kisiasa, na badala yake watazame mienendo yao wa kuaibisha kuhusu haki za binadamu.

Kanani Chafi amesema serikali ya Marekani na wenzake wengi wanaodai kutetea haki za binadamu katika nchi za Magharibi wanalaaniwa katika mahakama ya dhamiri ya binadamu kutokana na rekodi zao za kutia aibu za ukiukaji wa haki za binadamu.