Amir-Abdollahian: Uingiliaji wa Ufaransa katika masuala ya ndani ya Iran haukubaliki
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i91944-amir_abdollahian_uingiliaji_wa_ufaransa_katika_masuala_ya_ndani_ya_iran_haukubaliki
Akizungumza karibuni na Catherine Collona Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Ufaransa, Hossein Amir- Abdollahian Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amekosoa hatua za nchi hiyo za kuingilia masuala ya ndani ya Iran.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 21, 2022 03:58 UTC
  • Amir-Abdollahian: Uingiliaji wa Ufaransa katika masuala ya ndani ya Iran haukubaliki

Akizungumza karibuni na Catherine Collona Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Ufaransa, Hossein Amir- Abdollahian Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amekosoa hatua za nchi hiyo za kuingilia masuala ya ndani ya Iran.

Amir-Abdollahian ameandika katika ukurasa wake wa twitter kuhusu mazungumzo aliyofanya na Waziri mwenzake wa Mambo ya Nje wa Ufaransa pambizoni mwa Mkutano wa Baghdad-2 huko Jordan kuwa katika mazungumzo hayo amekosoa hatua ya Ufaransa ya kuingilia masuala ya ndani ya Iran na kulitaja jambo hilo kuwa lisilokubalika.  

Washiriki wa Mkutano wa Baghdad-2 mjini Amman, Jordan 

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran kabla ya hapo alikutana na kufanya mazungumzo na Josep Borrell Mjumbe wa ngazi ya juu na Mkuu wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya na akasema mazungumzo yao yalikuwa ya wazi, ya kirafiki na yenye kujenga. 

Hossein Amir-Abdollahian Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran juzi usiku aliwasili Amman, mji mkuu wa Jordan kwa lengo la kushiriki Mkutano wa Baghdad-2. 

Mkutano huo ulifanyika jana mjini Amman kwa kuhudhuriwa na nchi jirani na Iraq. Bahrain, Oman, Misri, Saudi Arabia, Imarati, Qatar, Uturuki, Iran, Iraq na Ufaransa ni miongoni mwa nchi zilizoshiriki mkutano huo.