-
Raia wa Uingereza waliokamatwa Iran washtakiwa kwa ujasusi
Feb 18, 2025 23:28Msemaji wa Idara ya Mahakama ya Iran amesema kuwa raia wawili wa Uingereza waliokamatwa hivi karibuni katika mji wa Kerman, kusini mashariki mwa nchi, wameshtakiwa kwa kufanya ujasusi kwa niaba ya mashirika ya kijasusi ya Magharibi.
-
Umuhimu wa maandamano makubwa ya Siku ya Kimataifa ya Quds
Feb 18, 2025 23:24Mkuu wa Makao Makuu ya Intifada na Siku ya Kimataifa ya Quds nchini Iran, Brigedia Jenerali Ramezan Sharif, amesisitiza umuhimu wa kupanga na kufanya juhudi za kufanikisha maandamano makubwa katika Siku ya Kimataifa ya Quds mwaka huu.
-
Kushiriki Iran katika "Mkutano wa Nchi za Bahari ya Hindi" kuna umuhimu gani?
Feb 18, 2025 23:05Duru ya Nane ya Mkutano wa Nchi za Bahari ya Hindi chini ya kauli mbiu "Kuelekea Upeo Mpya wa Ushirikiano wa Baharini" imefanyika tarehe 16 na 17 mwezi huu wa Februari huko Oman kwa kuhudhuriwa na viongozi wa ngazi ya juu wa nchi 20 wanachama. Oman, India na Singapore kwa pamoja zilikuwa wenyeji wa kongamano hilo.
-
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu: Mpango wa kijinga wa Marekani kuhusu Gaza hautafika popote
Feb 18, 2025 11:45Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, akiwapongeza wapiganaji wa Muqawama kwa ushindi wao katika Ukanda wa Gaza, amesisitiza kwamba kazi kubwa ya viongozi na wapiganaji wa Muqawama wa Palestina ipo katika "umoja na mshikamano" na "kusimama imara" dhidi ya adui, kuendesha mchakato mgumu wa mazungumzo, pamoja na uvumilivu na ustahimilivu wa wananchi, ambavyo vimeinua heshima ya Muqawama katika eneo.
-
Vikosi vya nchi kavu vya IRGC vyafanya maneva makubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa ya kujiandaa na vita
Feb 18, 2025 10:13Vikosi vya Nchi Kavu vya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC) vimeanza mazoezi makubwa zaidi ya kijeshi kuwahi kushuhudiwa vya kujiweka tayari kwa vita katika eneo la kusini-magharibi mwa nchi, ikiwa ni sehemu ya hatua za kuinua kiwango cha utayari wake wa kivita wa kukabiliana na vitisho vinavyoweza kutolewa na maadui.
-
Spika Ghalibaf: Iran inaunga mkono uthabiti nchini Sudan
Feb 18, 2025 04:08Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran), Mohammad Baqer Ghalibaf amesema Jamhuri ya Kiislamu inaunga mkono juhudi za kurejeshwa utulivu na uthabiti nchini Sudan, sanjari na kuundwa "utawala wa umoja" ambao utahakikisha kuwa taifa hilo lina mamlaka kamili ya kujitawala.
-
Tehran: Maajenti wa mauaji wanaituhumu Iran kukiuka haki
Feb 18, 2025 04:01Rais Masoud Pezeshkian wa Iran amesema Jamhuri ya Kiislamu inatuhumiwa kukiuka haki za binadamu na pande ambazo zinasababisha vifo na uharibifu katika pembe mbali mbali za dunia.
-
Iran kushiriki kwa ngazi ya juu katika mazishi za Shahidi Nasrallah
Feb 18, 2025 00:54Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Esmaeil Baghaei, amesema Iran itashiriki kwa ngazi ya juu katika mazishi ya aliyekuwa kiongozi wa harakati ya Muqawama ya Hizbullah nchini Lebanon, Sayyed Hassan Nasrallah.
-
Kiongozi Muadhamu: Vitisho vya adui dhidi ya nchi na wananchi wetu havijawa na natija
Feb 17, 2025 09:24Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, amesema kwamba maandamano makubwa ya watu wetu ya Bahman 22 ya maadhimisho ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu yalithibitisha kwamba vitisho vya maadui dhidi ya nchi yetu na watu wetu havijazaa matunda.
-
Araghchi: Himaya ya Yemen kwa Palestina ilikuwa na mchango muhimu katika ushindi wa Gaza
Feb 17, 2025 08:01Sayyid Abbas Araghchi, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, himaya ya Yemen kwa Palestina ilikuwa na mchango muhimu katika ushindi wa Gaza.