-
Araqchi: Kuvuka kipindi cha sasa kunahitaji kujiepusha na mifarakano
Dec 28, 2024 03:59Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran amewaambia maafisa wakuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu kwamba: Kuvuka kipindi hiki chenye taharuki nyingi katika eneo la Magharibi mwa Asia kunahitaji busara, ushirikishwaji, ushirikiano na kuepusha mizozo na kujitakia maslahi ya muda mfupi.
-
Rais wa Iran kutembelea Russia mwezi ujao kutia saini mkataba muhimu wa ushirikiano
Dec 27, 2024 23:39Rais Masoud Pezeshkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran atafanya ziara nchini Russia mwezi ujao ili kutia saini makubaliano ya ushirikiano wa kimkakati wa kina kati ya nchi hizo mbili.
-
Iran na Saudi Arabia kuimarisha uhusiano katika sekta ya teknolojia
Dec 27, 2024 23:14Rais wa Shirika la Teknolojia ya Habari na Mawasiliano la Iran na Rais wa Kamati ya Mawasiliano, Anga za Mbali na Teknolojia (CST) ya Saudi Arabia katika mkutano wa pamoja huko Riyadh wamesisitiza kuimarisha ushirikiano na kubadilishana uzoefu katika nyanja mbalimbali za teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA)
-
Ayatullah Siddiqi: Marekani ni mpangaji na mbunifu nambari moja katika uporaji na vita vyote
Dec 27, 2024 08:24Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya leo hapa mjini Tehran ameeleza kuwa, Marekani ndiye mpangaji mkuu katika mapinduzi yote, uporaji na vita na akasema: Jambo la lisilo na shaka ni kwamba suala la Syria kidhahiri lilionekana kuwa ni tukio lakini kwa ndani ilikuwa ni njama.
-
Rais Pezeshkian: Tunatazamia uhusiano wa kirafiki na nchi za kanda na ulimwengu
Dec 26, 2024 23:29Rais Masoud Pezeshkian wa Iran amesisitiza kuwa, Iran inatazamia kwa hamu kuwa na uhusiano wa kirafiki na nchi za eneo na dunia na inafanya hima kuhakikisha kunakuweko amani na usalama ndani na nje.
-
Esmaeil Baghaei: Shambulio dhidi ya gari la waandishi wa habari Gaza ni jinai ya kivita
Dec 26, 2024 23:28Esmaeil Baghaei, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, ameaani kulengwa kwa makusudi gari la waandishi wa habari karibu na kambi ya wakimbizi ya Nuseirat katikati mwa Ukanda wa Gaza, shambulio ambalo lilisababisha kuuawa waandishi wa habari watano.
-
Kuzaliwa Isa Masih, ukumbusho wa kupigania uadilifu; Ujumbe wa pongezi wa Wairani watumiaji wa mtandao wa X
Dec 26, 2024 06:57Watumiaji Wairani wa mtandao wa kijamii wa X wamekutaja kuzaliwa Nabii Isa Masih (Yesu Kristo), amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake, kuwa ni ukumbusho wa maadili ya kiroho ya ubinadamu.
-
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu awapongeza Wakristo kwa mnasaba wa kuzaliwa Isa Masih
Dec 26, 2024 03:24Ukurasa wa lugha ya Kiingereza wa Ofisi ya Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Ali Khamenei, katika mtandao wa kijamii wa X umechapisha ujumbe wake kwa mnasaba wa kumbukumbu ya kuzaliwa Nabii Isa Masih (as).
-
Iran yaitaka Ufaransa kutoa maelezo kuhusu mauaji ya raia 2 wa Iran nchini humo
Dec 26, 2024 03:18Tume ya Haki za Binadamu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imelaani mauaji ya raia wawili wa Iran nchini Ufaransa na kuitaka serikali ya nchi hiyo kutoa maelezo kuhusiana na jinai hiyo.
-
Ujumbe wa Rais Pezeshkian wa Iran kwa Papa Francis kwa mnasaba wa Krismasi
Dec 26, 2024 00:43Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika ujumbe wake kwa Papa Francis, amesema: Kusherehekea kuzaliwa kwa Nabii Isa Masih (AS) ni fursa ya kiroho ya kukumbusha Amri za Mwenyezi Mungu na mafundisho ya thamani ya manabii wote kwa ajili ya kutimiza haki, amani, na uhuru.