-
Iran yasema Krismasi ni fursa ya kujikumbusha wito wa Nabii Isa (AS) wa 'haki, amani'
Dec 26, 2024 00:42Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetoa salamu za Krismasi na Mwaka Mpya kwa Wakristo kote ulimwenguni, wakiwemo "wananchi wenzetu Wakristo" nchini Iran, ikisisitiza kwamba tukio hilo ni kumbusho la mafundisho ya Nabii Isa au Yesu Kristo (Amani Ya Mwenyezi Mungu Iwe Juu Yake-AS-) ya haki, amani na upendo.
-
Jeshi la Iran, IRGC kufanya mazoezi ya kijeshi yenye 'nguvu'
Dec 26, 2024 00:41Kamanda wa ngazi ya juu wa Iran ametangaza kwamba vikosi vya jeshi la Iran vitaandaa mazoezi tata ya kijeshi yenye na ambayo yatajumuisha Jeshi la Kitaifa (Artesh) na Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC).
-
Araghchi: Syria itashuhudia mabadiko makubwa
Dec 25, 2024 08:47Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, ni mapema mno kutabiri mustakabali wa Syria hasa kwa wale wanaodhani kuwa wameshinda.
-
Russia wavutiwa sana na bidhaa za nguo na ngozi za Iran
Dec 25, 2024 08:45Naibu wa Mkuu wa Mkoa wa Tehran katika masuala ya uratibu wa kiuchumi wa ametangaza habari ya kutiwa saini hati ya maelewano ya ushirikiano kati ya Iran na Russia katika masuala ya nguo na ngozi, baada ya wananchi wa Russia kuvutiwa sana na bidhaa za Iran.
-
Barua ya Iran kwa Baraza la Usalama baada ya Israel kukiri ilihusika na mauaji ya Ismail Haniyeh
Dec 25, 2024 08:37Amir Saeid Iravani, Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa jana Jumanne alimwandikia barua Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na Mkuu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa akisisitiza kwamba, Israel imebeba dhima ya kuhusika na mauaji ya Shahidi Ismail Haniyeh, mkuu zamani wa Idara ya Siasa ya harakati ya Hamas.
-
Iran yalaani vikali "kukiri bila ya aibu" Israel kuwa ndiyo iliyomuua kigaidi Ismail Haniya mjini Tehran
Dec 25, 2024 03:30Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imelaani vikali kauli ya utawala wa Kizayuni wa Israel ya "kukiri bila ya aibu" kuwa ndio uliomuua kigaidi Kiongozi wa Hamas Ismail Haniya mjini Tehran mapema mwaka huu, na kuyataja mauaji hayo kuwa ni "jinai ya kuchukiza mno".
-
Mshauri wa Kiongozi Mkuu: Iran imelisafisha hatua kwa hatua eneo na uwepo wa doa chafu la magaidi
Dec 25, 2024 03:26Mshauri wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imelisafisha hatua kwa hatua eneo na uwepo wa doa chafu la magaidi.
-
Araqchi: Makombora ya Yemen yamevuruga mahesabu ya Marekani na Israel
Dec 25, 2024 00:18Abbas Araqchi Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuwa usahihi wa makombora ya Yemen umevuruga kwa kiasi kikubwa mahesabu ya kimkakati ya muungano wa Israel na Marekani.
-
Iran: Tuko tayari kufungua tena ubalozi Syria, tunafanya mazungumzo na serikali ya Damascus
Dec 24, 2024 09:22Msemaji wa serikali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameeleza utayarifu wa Tehran kufungua tena ubalozi wake mjini Damascus, huku kukiwa na changamoto zinazoikabili Syria wiki mbili baada ya wanamgambo wa Hayat Tahrir al-Sham (HTS) kushika hatamu za nchi hiyo ya Kiarabu.
-
Makamu wa Rais wa Iran ahimiza kustawishwa uhusiano na Russia
Dec 24, 2024 03:23Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Iran amesema kuwa, viongozi wa ngazi za juu wa Iran wana nia ya kweli ya kustawisha uhusiano na Russia katika viwango vya juu.