-
Spika Qalibaf: Mkakati wa Marekani wa vitisho na kuvunja ahadi umefeli
Aug 07, 2026 03:38Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Mohammad Bagher Qalibaf, amekosoa miamala ya hivi karibuni ya Washington kama “diplomasia ya maigizo” isiyo na mashiko, akitangaza kuwa mkakati wa Marekani wa vitisho, kuvunja ahadi, na kusuka simulizi za uongo umefeli. Aidha amesisitiza kwamba Iran haitashiriki katika michezo hiyo ya kuigiza tena.
-
Waziri wa Ulinzi: Vikosi vya Iran vimesheheni silaha za kujibu mapigo kwa tishio lolote lile
Aug 07, 2026 03:36Kaimu Waziri wa Ulinzi wa Iran amesisitiza kuwa, kwa kutegemea utaalamu wa kiulinzi wa ndani ya nchi, Vikosi vya Ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu vimesheheni kila vinachohitaji ili kutoa jibu kwa tishio lolote lile.
-
Pezeshkian: Iran inajulikana kama nchi yenye nguvu na inayoheshimika; maadui wanalenga nembo za nguvu zake
Aug 06, 2026 11:08Rais Masoud Pezeshkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa licha ya changamoto zinazoikabili nchi, Iran inatambulika kimataifa kama taifa lenye nguvu na linaloheshimika sana, huku akitahadharisha kuwa maadui wa taifa hili wanajaribu kudhoofisha alama za nguvu zake.
-
IRGC: Watu 8 wenye silaha wenye mfungamano na makundi ya kigaidi watiwa nguvuni kusini-mashariki mwa Iran
Aug 06, 2026 11:06Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) kimetangaza kuwa kimewatia nguvuni watu wanane wenye silaha wenye mfungamano na makundi ya kigaidi katika mkoa wa Sistan na Baluchestan kusini-mashariki mwa Iran kufuatia oparesheni maalum mtawalia.
-
Mgawanyiko kati ya Nchi za Kiarabu za Ghuba ya Uajemi Kuhusu Vita vya Marekani dhidi ya Iran
Aug 06, 2026 05:45Kwa mujibu wa gazeti la The Wall Street Journal, nchi za Kiarabu katika eneo la Ghuba ya Uajemi bado zimegawanyika pakubwa kuhusu namna ya kushughulikia vita vya kichokozi na kulazimishwa dhidi ya Iran.
-
Pezeshkian: Iran itaunga mkono maamuzi yatakayochukuliwa na viongozi wa Palestina
Aug 06, 2026 03:53Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Masoud Pezeshkian, amesisitiza kuwa Jamhuri ya Kiislamu itaunga mkono mpango au uamuzi wowote utakaopitishwa na viongozi wa Palestina katika mchakato wa mazungumzo yanayoendelea, akithibitisha tena uungaji mkono thabiti wa Tehran kwa mapambano ya Palestina.
-
Waziri wa Afya wa Iran alaani shambulio la Marekani dhidi ya uwanja wa michezo wa Lamerd Februari mwaka huu
Aug 05, 2026 12:18Waziri wa Afya wa Iran kwa mara nyingine tena amelaani shambulio lililofanywa na jeshi la Marekani dhidi ya uwanja wa michezo katika mji wa Lamerd mwanzoni mwa mashambulizi ya nchii hiyo na utawala katili wa Israel mwezi Februari mwaka huu hapa nchini lililosababisha vifo kuwajeruhi raia kadhaa.
-
Gharama Halisi ya Vita vya Marekani dhidi ya Iran: Mara Nne ya Makadirio ya Pentagon
Aug 05, 2026 06:40Gazeti la Uingereza la The Telegraph limefichua kuwa gharama halisi ya vita vya Marekani dhidi ya Iran ni mara nne zaidi ya kiasi kilichotajwa na Pentagon.
-
Mamilioni ya Wairani washiriki Arubaini ya Imam Hussein, watoa wito wa kulipiza kisasi damu ya Kiongozi aliyeuawa shahidi
Aug 04, 2026 14:48Mamilioni ya Wairani wamekusanyika kote nchini kuadhimisha Arubaini ya Imam Hussein bin Ali (AS), ambayo inaashiria siku ya 40 baada ya kuuawa shahidi mjukuu huyo wa Mtume wetu Muhammad (SAW) huko Karbala nchini Iraq mwaka 61 Hijria.
-
Araqchi: Arubaini ya Imam Hussein ni onyesho kubwa la umoja wa kitaifa kati ya Iran na Iraq
Aug 04, 2026 10:35Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Sayyid Abbas Araqchi ameyataja matembezi ya Arubaini ya Imam Hussein baina ya miji miwili mitakatifu ya Najaf na Karbala nchini Iraq kuwa ni onyesho kubwa la umoja usiovunjika kati ya watu wa Iran na Iraq, akitilia mkazo viunganishi vikubwa vya kidini na kidugu vinavyoendelea kuimarisha uhusiano wa pande mbili.