-
Taarifa ya Wizara ya Ulinzi ya Iran ya kushukuru ujumbe wa Kiongozi wa Mapinduzi kuhusu mazungumzo ya Iran na Marekani
Jun 20, 2026 13:00Katika kujibu ujumbe wa Kiongozi muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kuhusu mazungumzo ya Iran na Marekani, Wizara ya Ulinzi na Msaada Kwa Jeshi la Iran imesisitiza katika taarifa kwamba: Siri ya mafanikio endelevu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni kufuata kamilifu na bila kusitasita amri na hatua za Amiri Jeshi Mkuu.
-
Waziri wa mambo ya ndani wa Pakistan arejea tena Tehran kujadili mazungumzo ya Iran na Marekani
Jun 20, 2026 12:10Syed Mohsin Raza Naqvi, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Pakistan amerejea tena Tehran kwa ajili ya kukutana na kuzungumza na viongozi wa ngazi za juu wa Iran, kuhusu suala la kuendeleza mazungumzo kati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Marekani.
-
Bunge la Iran: Ukiukaji wowote wa ahadi wa Marekani utakabiliwa na jibu kali
Jun 20, 2026 12:08Mwenyekiti wa Kamisheni ya Usalama wa Taifa na Siasa za Kigeni ya Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran ameandika katika akaunti yake ya mtandao wa kijamii kwamba: "Ukiukaji wowote wa ahadi utakaofanywa na Marekani au kujiondoa katika fremu kuu ya maelewano kutapelekea jeshi la Iran, kwa uungaji mkono wa taifa shupavu la Iran kutoa jibu kali, thabiti na la kuumiza zaidi dhidi ya adui huyo kuliko ilivyokuwa huko nyuma."
-
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran: Amani na uthabiti nchini Lebanon na eneo havitapatikana bila ya kukomeshwa uvamizi wa adui
Jun 20, 2026 12:05Katika mahojiano na televisheni ya Al Jazeera, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesisitiza kuwa: Washington lazima imzuie Netanyahu kuvuruga juhudi za maelewano kwa sababu hakuna amani wala utulivu wowote utakaopatikana Lebanon na katika eneo zima la Asia Magharibi bila kukomeshwa uvamizi na ukaliaji mabavu wa ardhi za nchi za eneo.
-
Trump: Kama nisingesimamisha vita na Iran, tungeachwa bila mafuta
Jun 20, 2026 11:47Katika mahojiano na chombo cha habari cha Marekani Axios, Rais Doland Trump wa Marekani amekiri hadharani kwamba hakuwa na budi ila kufanya mazungumzo na Iran kwa ajili ya kumaliza vita.
-
Iran yasitisha mazungumzo na Marekani nchini Uswisi baada ya Israel kuendeleza hujuma Lebanon
Jun 20, 2026 04:26Mazungumzo ya kidiplomasia kati ya Iran na Marekani nchini Uswisi, yaliyokusudiwa kuimarisha Hati ya Makubaliano (MoU) iliyosainiwa hivi karibuni, yameahirishwa.
-
IRGC: Tuko tayari kuwapa maadui ‘kichapo kikubwa zaidi’ ikiwa haki za Iran zitakiukwa
Jun 20, 2026 04:24Jeshi la Iran la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limethibitisha utayari wake wa kuwapa maadui “kichapo kikubwa cha kihistoria” iwapo wataendeleza madai yao ya kupita kiasi na kukiuka haki za taifa tukufu la Iran.
-
Walinzi wa mpaka wa Iran na Iraq washirikiana kuandaa marasimu ya Arbaeen
Jun 19, 2026 12:35Walinzi wa mpaka wa pamoja wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Jamhuri ya Iraq wamefanya vikao vya pamoja katika mpaka wa eneo la Mehran katika mkesha wa kuanza rasmi wimbi kubwa la mazuwwar wa Muharram na Arbaeen.
-
Imam wa Swala ya Ijumaa mjini Tehran: Utawala wa Marekani hauaminiki hata kidogo
Jun 19, 2026 12:27Huku akisema kuwa, nguvu ni matunda ya subira mitaani, medani ya vita na diplomasia kwa pamoja, Khatibu wa Swala ya Ijumaa ya mjini Tehran amesisitiza kuwa: 'Leo utawala wa Marekani hauaminiki hata kidogo.'
-
Mkataba wa Maelewano na Iran: Mwisho wa nguvu ya Dola la Marekani
Jun 19, 2026 12:25Tucker Carlson, mtangazaji na mchambuzi mashuhuri wa Marekani, amesema katika taarifa kuhusu makubaliano ya hivi karibuni kati ya Iran na Marekani kwamba makubaliano hayo yamemaliza kikamilifu nguvu, kiburi, majigambo na ubabe wa Marekani katika ngazi ya kimataifa na kuipelekea ikiri rasmi hadharani kwamba Iran ni mchezaji muhimu mwenye maamuzi huru, na kwamba hilo pekee limebadilisha kila kitu katika mtazamo wa kisiasa na kijeshi.