-
Jumuiya ya Shanghai yalaani shambulio la Israel dhidi ya Iran
Nov 02, 2024 23:03Wawakilishi wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai wametoa taarifa na kulaani vikali hatua ya kichokozi ya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya vituo vya kijeshi vya Iran.
-
Imam Khamenei: Marekani na Israel bila shaka, zitapokea 'jibu la kuvunja meno'
Nov 02, 2024 07:49Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu mapema leo ameeleza sababu za msingi za mapambano ya taifa la Iran yanayoendelea kwa takriban miaka 70 dhidi ya dhulma na sera za kupenda kujitanua za Marekani, na kusisitiza kuwa: Katika njia hiyo ya ushindi, utawala wa Kizayuni na Marekani watapewa jibu kali kwa hatua yoyote dhidi ya taifa la Iran.
-
Kuendelea hatua na misimamo ya undumakuwili ya Marekani dhidi ya Iran
Nov 02, 2024 07:45Rais Joe Biden wa Marekani jana Ijumaa aliwatumia barua wakuu wa bunge la wawakilishi na seneti ambapo amerefusha kwa mwaka mmoja mwingine muda wa hali ya hatari kitaifa kuhusu Iran. Biden amechukua hatua hii katika miezi yake ya mwisho akiwa White House na kabla ya kufanyika uchaguzi wa Rais wa Marekani tarehe 5 mwezi huu wa Novemba.
-
Kharrazi: Kuna muelekeo wa Iran kuongeza umbali wa masafa yatakakofika makombora yake
Nov 02, 2024 04:11Kamal Kharrazi, Mkuu wa Baraza la Kistratejia la Mahusiano ya Nje la Iran amesema, kuna muelekeo wa Jamhuri ya Kiislamu kuongeza umbali wa masafa yatakakofika makombora yake, akionya kuwa Tehran inaweza kubadilisha mwongozo wake wa kijeshi iwapo itakabiliwa na kitisho cha kuhatarisha uwepo wake.
-
Pezeshkian: Iran imeazimia kuimarisha uhusiano na Algeria
Nov 01, 2024 23:30Rais wa Iran Masoud Pezeshkian ameipongeza Algeria kwa kuadhimisha miaka 70 ya mapinduzi yake, akielezea utayarifu wa Iran wa kuimarisha uhusiano na nchi hiyo ya Kiarabu katika nyuga mbali mbali.
-
China: Tunaunga mkono kuheshimiwa usalama wa kitaifa wa Iran
Nov 01, 2024 23:27Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya China imetangaza kuwa, inaunga mkono juhudi za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran za kudumisha uthabiti na usalama wake wa taifa dhidi ya aina yoyote ya ugaidi.
-
Sheikh Kazem Siddiqi: Iran ina haki kujibu chokochoko za utawala wa Kizayuni wa Israel
Nov 01, 2024 10:04Khatibu wa Swala ya Ijumaa iliyosaliwa leo hapa mjini Tehran amesema kuhusu mashambulizi ya hivi karibuni ya utawala wa Kizayuni dhidi ya Iran kwamba, haki ya kujibu uchokozi huo imehifadhiwa kwa mujibu wa Kifungu cha 51 cha Mkataba wa Umoja wa Mataifa.
-
Kamanda wa IRGC: Israel itakabiliwa na jibu lisilofikirika
Nov 01, 2024 07:02Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran (IRGC) ameionya Israel kwamba, itapata jibu kali na zito kwa kitendo chake cha hivi karibuni cha uchokozi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu; jibu ambalo halifikiriki wala kutasawirika.
-
Qaani: Kikosi cha Quds cha IRGC kitakuwa pamoja na Hizbullah hadi kuangamizwa Uzayuni
Nov 01, 2024 03:41Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran amempongeza Sheikh Naim Qassim kwa kuchaguliwa kuwa Katibu Mkuu mpya wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon na kusema: Kikosi cha Quds kitakuwa pamoja na Hizbullah hadi utakapotokomezwa mti habithi wa Uzayuni na kukombolewa Palestina na Quds Tukufu.
-
Rais Pezeshkian: Umoja utawafanya Waislamu kuwa na nguvu kubwa
Oct 31, 2024 22:57Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza juu ya umoja baina ya nchi za Kiislamu na kusema: Iwapo tutaweza kufikia umoja katika nyanja za kiuchumi, kisiasa na kijamii, tunaweza kuwa nguvu kubwa katika eneo la Asia Magharibi, na katika hali hii Marekani haiwezi kutuwekea vikwazo.