-
Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Iran na Misri wafanya mazungumzo kuhusu chokochoko mpya za Israel dhidi ya Iran
Oct 28, 2024 03:20Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri jana Jumapili ilitoa taarifa na kusema kuwa, Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo, Badr Abdelatty amefanya mazungumzo ya simu na waziri mwenzake wa Iran, Sayyid Abbas Araghchi na kujadiliana naye kuhusu shambulio la Israel la siku ya Jumamosi dhidi ya baadhi ya maeneo ya Iran.
-
Iran yaliandikia barua Baraza la Usalama kuhusu shambulio la kigaidi kusini mashariki mwa nchi
Oct 27, 2024 23:28Balozi wa Kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa ameliandikia barua Baraza la Usalama la Umoja huo na kulitaka litoe azimio la kulaani shambulio la kigaidi la genge linalojiita "Jeysh al Adl" katika mkoa wa Sistan na Baluchistan wa kusini mashariki mwa Iran.
-
Araghchi: Iran itatoa majibu kwa Israel katika wakati itakaoona unafaa
Oct 27, 2024 23:27Sayyid Abbas Araghchi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesisitiza kuwa, ni haki ya Jamhuri ya Kiislamu kujibu uchokozi wa utawala wa Kizayuni na itatoa majibu dhidi ya Israel katika muda itakaoona unafaa.
-
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu: Utawala wa Kizayuni umefanya makosa ya kimahesabu
Oct 27, 2024 08:50Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema: Wakuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel wamefanya mahesabu potofu kuhusu Jamhuri ya Kiislamu kwa sababu hawawafahamu vijana na wananchi wa Iran na bado hawajaweza kuelewa ipasavyo nguvu, uwezo, uvumbuzi na irada ya taifa hili.
-
Baraza la Usalama kujadili hatua za uchokozi za Israel dhidi ya Iran kesho Jumatatu
Oct 27, 2024 08:19Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limesema kuwa kesho Jumatatu litaitisha kikao kujadili mashambulizi ya utawala wa Kizayuni dhidi ya Iran.
-
Mwandishi wa Uingereza: Wairani wanafanyia maskhara shambulio dhaifu la Israel
Oct 27, 2024 06:17Mwandishi wa Uingereza ameutaja “uchokozi wa kimaonyesho” wa utawala wa Kizayuni wa Israel katika ardhi ya Iran kuwa ni dhihaka kwa watu wa nchi hiyo.
-
Iran: Umoja wa Ulaya unapendelea maslahi yake kuliko sheria za kimataifa
Oct 27, 2024 04:36Katika kujibu kauli ya Umoja wa Ulaya kufuatia uchokozi wa utawala ghasibu wa Israel dhidi ya Iran, ubalozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini Brussels umesema kuwa umoja huo unapendelea zaidi maslahi yake binafsi kuliko sheria za kimataifa.
-
Barua ya Iran kwa UN: Hatua za utawala wa Kizayuni ni tishio kuu kwa amani na usalama wa dunia
Oct 27, 2024 04:25Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amemwandikia barua Mwenyekiti wa Baraza la Usalama na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kufuatia mashambulizi ya jana ya utawala wa Kizayuni dhidi ya vituo vya kijeshi vya Iran na kusisitiza kuwa: Hatua za Tel Aviv ni tishio kubwa kwa amani na usalama wa kimataifa.
-
Uwezekano wa kuratibiwa uchokozi wa utawala wa Israel na shambulio la kigaidi la Jaish al-Dhulm
Oct 27, 2024 04:13Tathmini ya jinai za utawala wa Kizayuni katika miaka ya hivi karibuni, inatoa uwezekano wa kuwepo uratibu wa hatua ya kichokozi ya hivi karibuni ya utawala huo dhidi ya Iran na shambulio la kigaidi lililotekelezwa na magaidi wa Jeish Dhulm katika eneo la kusini mashariki mwa nchi.
-
Rais Pezeshkian: Wairani watajibu chokochoko za maadui dhidi ya nchi yao
Oct 26, 2024 23:40Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian ametoa rambirambi zake kufuatia kuuawa shahidi maafisa usalama wa nchi hii katika mashambulizi ya kichokozi ya jana Jumamosi ya utawala wa Kizayuni na kundi la kigaidi linaloungwa mkono na maajinabi.