-
Risasi za Israel zapatikana katika miili ya watoto waliouawa wakati wa ghasia hivi karibuni Iran
Jan 22, 2026 07:03Risasi za kiwango cha kijeshi zinazohusishwa na jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel zimepatikana katika uchunguzi wa kitabibu wa miili ya watoto waliouawa na magaidi wakati wa ghasia za hivi karibuni zilizochochewa na serikali za kigeni nchini Iran
-
Jeshi la Iran la IRGC laionya Marekani na Israel dhidi ya makosa yoyote ya kimahesabu
Jan 22, 2026 07:03Kamanda Mkuu wa Jeshi la Iran la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amewaonya maadui dhidi ya kufanya makosa yoyote ya kimahesabu, akisisitiza kwamba vikosi vyake viko tayari kutekeleza maagizo ya Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Seyyed Ali Khamenei.
-
Kamanda mwandamizi wa Jeshi la Iran amuonya vikali Trump
Jan 22, 2026 03:26Kamanda wa ngazi ya juu wa jeshi la Iran amemuonya vikali Rais Donald Trump wa Marekani kufuatia matamshi yake ya hivi karibuni ya vitisho dhidi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei.
-
Iran yatangaza idadi ya waliouawa katika ghasia zilizochochewa na maajinabi
Jan 22, 2026 02:32Wakfu wa Mashahidi na Maveterani wa Iran umetangaza katika taarifa kwamba, "katika vitendo vya hivi karibuni vya ugaidi vilivyoungwa mkono na Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel, watu 3117 walipoteza maisha yao, wakiwemo raia na maafisa usalama."
-
Araghchi aionya Marekani: Shambulio lolote jipya dhidi ya Iran litakabiliwa na jibu kali
Jan 21, 2026 23:39Sayyid Abbas Araghchi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesisitiza kwamba uchokozi wowote mpya wa kijeshi dhidi ya Iran utakabiliwa na jibu kali na la uhakika.
-
Bahreini: Iran haitafumbia macho katu haki yake ya kurutubisha urani kwa matumizi ya amani
Jan 21, 2026 07:12Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Ofisi ya Umoja wa Mataifa mjini Geneva amesisitiza kwamba, taifa hili halitafumbia macho katu haki yake ya kurutubisha urani kwa ajili ya matumizi ya amani.
-
Kwa nini Iran inatilia mkazo kuhusu haki yake ya kurutubisha urani kwa ajili ya malengo ya amani?
Jan 21, 2026 06:32Iran imetangaza kuwa abadan haitaacha haki yake ya kurutubisha madini ya urani kwa malengo ya kiraia.
-
Araqchi: Tatizo la sasa la Ulaya ni matokeo ya usaliti wake wa huko nyuma dhidi ya Iran
Jan 21, 2026 04:18Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araqchi, amesema Ulaya sasa inasumbuliwa na matokeo ya usaliti wake wa zamani kwa Iran na inakabiliwa na unyanyasaji kama huo kutoka kwa Marekani.
-
"Jeshi la Iran litakata 'mkono wowote wa chokochoko' dhidi ya Kiongozi Muadhamu"
Jan 20, 2026 23:44Afisa wa ngazi ya juu wa Jeshi la Iran amepuuzilia mbali vitisho vya maneno vya hivi karibuni vya Rais wa Marekani Donald Trump, akionya kwamba, hatua yoyote ya uadui itakayoelekezwa kwa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei itakabiliwa na kisasi kikubwa cha kijeshi.
-
Zaidi ya magaidi 470 na vinara wa ghasia wakamatwa katika mikoa kadhaa ya Iran
Jan 20, 2026 06:53Maafisa wa usalama na taasisi za ujasusi za Iran zimewakamata zaidi ya watu 470 katika mikoa mitatu, waliotambuliwa kama watu muhimu na vinara wa wimbi la hivi karibuni la machafuko ya vurugu na harakati za kigaidi zinazohusiana na mitandao inayoungwa mkono na madola ya kigeni.