Iran yakosoa upotoshaji wa CENTICOM kuhusu mauaji ya halaiki ya Minab
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i138516-iran_yakosoa_upotoshaji_wa_centicom_kuhusu_mauaji_ya_halaiki_ya_minab
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amekadhibisha matamshi ya Kamandi Kuu ya Marekani (CENTCOM) kuhusu mashambulizi ya ya makombora yaliyofanywa katika shule ya msingi ya Shajareh Tayyebeh huko Minab kusini mwa Iran na kuyataja kuwa "yasiyo na msingi".
(last modified 2026-05-21T12:34:11+00:00 )
May 21, 2026 04:36 UTC
  • Shule ya msingi ya Minab, Iran iliyoshambuliwa na Marekani
    Shule ya msingi ya Minab, Iran iliyoshambuliwa na Marekani

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amekadhibisha matamshi ya Kamandi Kuu ya Marekani (CENTCOM) kuhusu mashambulizi ya ya makombora yaliyofanywa katika shule ya msingi ya Shajareh Tayyebeh huko Minab kusini mwa Iran na kuyataja kuwa "yasiyo na msingi".

Ismail Baqaei amesema kuwa, Marekani inajaribu kuepa kubeba dhima ya mauaji ya zaidi ya wanafunzi 170 na walimu wao katika jinai hiyo ya kutisha.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran mapema Jumatano alituma ujumbe katika akaunti yake ya X kwamba: Madai yanayotolewa na Kamanda Kuu ya Marekani (CENTCOM) kwamba shule ya msingi ya Shajareh Tayyebeh iliyoshambuliwa huko Minab ilikuwa ndani ya 'kituo cha kurusha makombora' ni uzushi usio na msingi na uongo wa kutisha."

Katika siku ya kwanza ya vita vya kulazimishwa vilivyoanzishwa na na muungano wa kijeshi wa Marekani na Israel Februari 28 mwaka huu makombora ya Tomahawk ya Marekani yalishambulia shule ya msingi ya wasichana ya Shajareh Tayyebeh huko Minab, kusini mwa Iran, na kuua takriban watu 175, wengi wao wakiwa wanafunzi wa shule hiyo.

Baqaei ameeleza haya baada ya Admeri Brad Cooper Kamanda wa CENTCOM kudai katika kikao cha kamati ya Bunge kwamba shule hiyo ilikuwa karibu na kambo ya makombora ya Kruzi ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC).

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesisitiza kuwa "Upotoshaji huu wa fedheha wa Marekani ni jaribio la wazi la kuficha ukweli mchungu wa mashambulizi hayo ya Februari 28, ambayo yalisababisa vifo vya kusikitisha vya zaidi ya watoto wa shule 170 na walimu wao,". Kulenga taasisi hai ya elimu huku wanafunzi wakiwa katikati ya masomo ni ukiukaji mkubwa wa sheria ya kimataifa ya binadamu na ni jinai ya wazi ya kivita.