-
Katibu Mkuu wa UN alaani vikali hatua ya Israel ya kubomoa majengo ya UNRWA Quds Mashariki
Jan 21, 2026 07:07Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amelaani kitendo cha vikosi vya utawala wa kizayuni wa Israel cha kubomoa majengo yaliyomo ndani ya eneo la makao makuu ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Palestina (UNRWA) katika mji wa Baitul Muqaddas Mashariki unaokaliwa kwa mabavu.
-
Kwa nini Iran inatilia mkazo kuhusu haki yake ya kurutubisha urani kwa ajili ya malengo ya amani?
Jan 21, 2026 06:32Iran imetangaza kuwa abadan haitaacha haki yake ya kurutubisha madini ya urani kwa malengo ya kiraia.
-
Serikali ya Somalia imechukua hatua gani katika kukabiliana na kujitenga kwa Somaliland?
Jan 21, 2026 04:28Kufuatia kuongezeka harakati za watu wanaotaka kujitenga huko Somaliland baada ya kutambuliwa rasmi na utawala wa Kizayuni wa Israel, serikali ya Somalia imechukua hatua mpya za kukabiliana na harakati hizo katika eneo hilo.
-
Araqchi: Tatizo la sasa la Ulaya ni matokeo ya usaliti wake wa huko nyuma dhidi ya Iran
Jan 21, 2026 04:18Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araqchi, amesema Ulaya sasa inasumbuliwa na matokeo ya usaliti wake wa zamani kwa Iran na inakabiliwa na unyanyasaji kama huo kutoka kwa Marekani.
-
Mahakama ya Ubelgiji yafungua tena kesi ya mauaji ya Patrice Lumumba
Jan 21, 2026 04:17Familia ya shujaa wa uhuru wa Kongo, Patrice Lumumba, ilisema jana Jumanne kwamba inatumai kupata haki, huku mahakama ya Ubelgiji ikizingatia kumfungulia mashtaka mshukiwa pekee aliyebakia hai hadi sasa kuhusu mauaji ya mwaka 1961 ya Lumumba.
-
Zilzala ya kisiasa yatishia Kombe la Dunia 2026... Ujerumani yadokeza kususia au kufutwa mashindano hayo
Jan 21, 2026 04:17Mashindano ya Kombe la Dunia 2026, yaliyopangwa kufanyika msimu ujao wa joto Amerika Kaskazini, yanakabiliwa na tishio lisilo la kawaida, baada ya sauti nyingi nchini Ujerumani kuibuka zikitaka kususiwa Kombe la Dunia la mpira wa miguu," na hata kutoa wito wa kufutwa kabisa mashindano hayo ili kupinga sera za Rais wa Marekani, Donald Trump.
-
Gazeti la New York Times laorodhesha "uongo" wa Rais Trump katika mwaka mzima
Jan 21, 2026 04:15Gazeti la New York Times linaamini kwamba katika mwaka wa kwanza wa muhula wake wa pili, Rais wa Marekani Donald Trump amesema uongo mwingi, kutoa madai yasiyo na msingi na upotoshaji ili kuhalalisha mabadiliko na kudanganya kuhusu mafanikio katika maeneo ya uchumi, uhamiaji na kadhalika.
-
Polisi wa Nigeria wakanusha ripoti za utekaji nyara kanisani huko Kaduna
Jan 21, 2026 04:14Polisi wa Nigeria wamekanusha ripoti kwamba waumini walitekwa nyara makanisani katika jimbo la Kaduna siku ya Jumapili iliyopita, wakisisitiza kwamba hakuna shambulio kama hilo lililotokea.
-
"Jeshi la Iran litakata 'mkono wowote wa chokochoko' dhidi ya Kiongozi Muadhamu"
Jan 20, 2026 23:44Afisa wa ngazi ya juu wa Jeshi la Iran amepuuzilia mbali vitisho vya maneno vya hivi karibuni vya Rais wa Marekani Donald Trump, akionya kwamba, hatua yoyote ya uadui itakayoelekezwa kwa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei itakabiliwa na kisasi kikubwa cha kijeshi.
-
Afya ya kiongozi mkongwe wa upinzani nchini Uganda aliyeko gerezani yadaiwa kuzorota
Jan 20, 2026 23:09Chama cha upinzani nchini Uganda cha People’s Front for Freedom kimesema katika taarifa kwamba afya ya kiongozi mkongwe wa upinzani nchini humo Kizza Besigye “iko katika hali mbaya na inaendelea kudhoofika,” na kutoa mwito wa kutaka aruhusiwe kukaguliwa na madaktari wake binafsi pamoja na familia yake.