-
Maandamano yazuka katikati ya jiji la Los Angeles kulaani mauaji ya mwanamke
Jan 11, 2026 07:26Watu wenye hasira wanaendelea kuandamana nchini Marekani ikiwa ni pamoja na mitaa ya jiji la Los Angeles kupinga hatua ya maafisa wa Trump kushambulia kiholela raia na kuua kwa uchache mtu mmoja na kujeruhi wengine wawili.
-
Walowezi wanatumia watoto kusumbua jamii za Wapalestina Ukingo wa Magharibi
Jan 11, 2026 07:25Walowezi wa Kizayuni mara kwa mara wanatumia vikundi vya watoto wa Kizayuni kuzisumbua na kuzifanyia maudhi jamii za Wapalestina na kuharibu maeneo yao ya kilimo katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan unaokaliwa kwa mabavu na Wazayuni hao.
-
Denmark na mashinikizo ya Marekani yanayozidi kuongezeka ya kutaka kuinyakua Greenland
Jan 11, 2026 05:54Sasa hivi kuliko wakati mwingine wowote Denmark inaandamwa na mashinikizo makali ya Marekani ya kutaka kuinyang'anya nchi hiyo kisiwa cha Greenland.
-
Somalia: Israel kuwahamishia kwa nguvu Wapalestina Somaliland ni kinyume cha sheria za kimataifa
Jan 11, 2026 03:26Waziri wa Ulinzi wa Somalia, Ahmed Moalim Fiqi, ameishutumu Israel kwa kupanga kuwahamisha kwa nguvu Wapalestina wa Ukanda wa Gaza na kuwapeleka katika eneo lililojitenga la Somaliland, akiukashifu mpango huo alioutaja kuwa ni "ukiukaji mkubwa" wa sheria za kimataifa.
-
Waziri Araghchi aanika nafasi ya Marekani, Israel katika ghasia za Iran
Jan 11, 2026 03:25Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Sayyid Abbas Araghchi amezionya vikali Marekani na utawala haramu wa Israel juu ya matokeo mabaya ya uchochezi na uungaji mkono wao kwa wafanya fujo na wazua rabsha hapa nchini, akisisitiza kuwa Washington na Tel Aviv zinataka kuyageuza maandamano ya kiuchumi ya wananchi wa Iran kuwa machafuko na ghasia.
-
Wairani kufanya maandamano kote nchini kupinga ghasia na fujo
Jan 11, 2026 03:06Baraza la Uratibu wa Uenezi wa Kiislamu la Iran limetangaza kuwa, wananchi Waislamu wa Jamhuri ya Kiislamu kesho Jumatatu watafanya maandamano katika pembe zote za nchi kulaani ghasia na fujo zilizochochewa hapa nchini na Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Waziri wa Ulinzi wa Pakistan: US ilipaswa kumteka Netanyahu, si Maduro
Jan 11, 2026 03:04Waziri wa Ulinzi wa Pakistan amesema "Marekani inapaswa kumteka nyara na kumshtaki katika mahakama yake yoyote ile Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel, Benjamin Netanyahu, ikiwa Washington ni rafiki halisi wa ubinadamu."
-
Ethiopia yaanza ujenzi wa 'uwanja mkubwa zaidi wa ndege barani Afrika'
Jan 11, 2026 03:03Ethiopia imezindua ujenzi wa 'uwanja mkubwa zaidi wa ndege barani Afrika' utakaogharimu dola bilioni 12.5 za Marekani.
-
Rais Pezeshkian asisitiza azma ya Iran ya kutekeleza makubaliano yake na Oman
Jan 11, 2026 00:48Rais Masoud Pezeshkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza umuhimu wa kupanua na kuendeleza uhusiano na majirani na nchi za Kiislamu kama kipaumbele cha kimkakati cha Tehran.
-
Setilaiti ya kwanza ya rada ya Iran kuzinduliwa karibuni hivi
Jan 11, 2026 00:23Mkuu wa Shirika la Anga za Mbali la Iran ametangaza kuwa: Setilaiti ya kwanza ya rada ya Iran ambayo imebuniwa na kutengenezwa na Shirika la Anga za Mbali la Sairan la Iran itazinduliwa karibuni hivi.