Setilaiti ya kwanza ya rada ya Iran kuzinduliwa karibuni hivi
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i135350-setilaiti_ya_kwanza_ya_rada_ya_iran_kuzinduliwa_karibuni_hivi
Mkuu wa Shirika la Anga za Mbali la Iran ametangaza kuwa: Setilaiti ya kwanza ya rada ya Iran ambayo imebuniwa na kutengenezwa na Shirika la Anga za Mbali la Sairan la Iran itazinduliwa karibuni hivi.
(last modified 2026-01-11T05:38:03+00:00 )
Jan 11, 2026 03:53 UTC
  • Setilaiti ya kwanza ya rada ya Iran kuzinduliwa karibuni hivi
    Setilaiti ya kwanza ya rada ya Iran kuzinduliwa karibuni hivi

Mkuu wa Shirika la Anga za Mbali la Iran ametangaza kuwa: Setilaiti ya kwanza ya rada ya Iran ambayo imebuniwa na kutengenezwa na Shirika la Anga za Mbali la Sairan la Iran itazinduliwa karibuni hivi.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Fars, Hassan Salarieh, mkuu wa Shirika la Anga za Mbali la Iran amesema hayo wakati alipokuwa akitazama picha za setilaiti ya Paya ikipita juu ya anga ya Iran katika Kampuni ya Viwanda vya Kielektroniki vya Iran (Sairan), na kuwaambia waandishi wa habari kwamba: Tangu setilaiti ya Paya ilipowekwa kwenye obiti pamoja na setilaiti mbili "Zafar" na "Kowsar"  kila siku kunafanyika mawasiliano na setilaiti hizo katika vituo vya ardhini.

Amesema: Mifumo yote ya setilaiti hizo imepasi vizuri katika majariibio yake ya awali na sasa zimeingia katika awamu ya uendeshaji; kwa maana kwamba utendaji wa kila mfumo mdogo katika obiti umethibitishwa kwa undani.

Aidha Mkuu wa Shirika la Anga za Mbali la Jamhuri ya Kiislamu ya Irian ametangaza habari njema kwa kusema: Setilaiti ya kwanza ya rada ya Iran iliyotengenezwa na kubuniwa na Shirika la Anga za Mbali la Sairan na ambayo itazinduliwa karibuni hivi itakuwa ni mafanikio mengine makubwa kwa taifa la Iran. Amesema, tutashuhudia huduma za setilaiti hiyo baada ya uzinduzi. Pia miradi mingine mingi inayohusiana na usanifu, ubunifu na uzalishaji wa setilaiti inaendelea nchini Iran kupitia Taasisi ya Utafiti wa Anga za Mbali ya Iran na Shirika la Anga za Mbali la Sairan.