-
Ripoti: US inaishinikiza Israel iuondoe mlima wa kifusi uliozagaa Ghaza baada ya miaka 2 ya vita
Dec 12, 2025 06:40Marekani imeitaka Israel ibebe jukumu la kuondoa vifusi vikubwa vilivyotapakaa kwenye kila pembe ya Ukanda wa Ghaza baada ya zaidi ya miaka miwili ya vita vya kinyama na mauaji ya kimbari iliyofanya dhidi ya Wapalestina wa eneo hilo, pamoja na uharibifu mkubwa uliosababishwa na mashambulizi yake ya anga na matingatinga ya kivita. Hayo yameelezwa na toleo la Alkhamisi la gazeti la kizayuni la Yedioth Ahronoth.
-
UN yasema Marekani inapaswa kuondoa vikwazo dhidi ya wanadiplomasia wa Iran
Dec 12, 2025 03:29Umoja wa Mataifa umesisitiza kuwa Marekani inalazimika kuwawezesha wanadiplomasia wa Iran walioidhinishwa kutekeleza majukumu yao bila vizuizi, ukikumbusha msimamo wa taasisi hiyo kwamba Washington, kama nchi mwenyeji, ina wajibu wa kuruhusu harakati zisizo na mipaka kwa maafisa wote wa kidiplomasia walioko katika makao makuu ya UN.
-
Rais Samia apokea hati za utambulisho za balozi wa Iran nchini Tanzania
Dec 12, 2025 03:28Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, jana alipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa mabalozi wapya watano walioteuliwa kuziwakilisha nchi zao, katika hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino, mkoani Dodoma.
-
UN: Mapigano yanashadidi mashariki mwa DRC
Dec 12, 2025 03:26Mapigano yanayoendelea kukithiri mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) yamesababisha vifo vya zaidi ya raia 70, kuwafurusha makwao zaidi ya watu 200,000 na kuwakosesha maelfu ya watu msaada wa chakula.
-
Guterres atoa wito kwa Eritrea na Ethiopia kuheshimu makubaliano ya mpaka
Dec 12, 2025 03:25Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ijumaa, amezitaka Eritrea na Ethiopia kurejea kwenye dhamira ya makubaliano yaliyomaliza rasmi uhasama kati ya mataifa hayo mawili ya Pembe ya Afrika miaka 25 iliyopita, akionya kuwa mvutano unaoibuka upya unaweza kuhatarisha amani ya eneo.
-
Khan: Uingereza ilitishia kukata ufadhili wa ICC kutokana na waranti wa kukamatwa Netanyahu
Dec 12, 2025 03:24Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC), Karim Khan, amesema serikali ya Uingereza ilitishia kuikatia mahakama hiyo ufadhili na kujiondoa kwenye Mkataba wa Roma uliounda taasisi hiyo, endapo jopo la majaji lingeendelea na mpango wa kutoa waranti wa kukamatwa kwa waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu.
-
Rais Pezeshkian:Iran na Kazakhstan ziimarishe uhusiano ili kukabiliana na Marekani
Dec 11, 2025 23:34Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian, amesema kuwa Iran na Kazakhstan zinapaswa kuimarisha uhusiano wa karibu ili kukabiliana na ubeberu Marekani.
-
Sudan Kusini yatuma wanajeshi kulinda eneo muhimu la mafuta la Heglig nchini Sudan
Dec 11, 2025 23:11Sudan Kusini imetuma wanajeshi wake katika nchi jirani ya Sudan kwa lengo kulinda kisima cha kimkakati cha mafuta cha Heglig karibu na mpaka. Haya yamebainishwa jana Alhamisi na Mkuu wa jeshi la nchi siku chache baada ya Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) kulidhibiti eneo hilo.
-
Umoja wa Mataifa: Hali ya kibinadamu Gaza ni mbaya
Dec 11, 2025 23:10Umoja wa Mataifa umeonya kuhusu kuongezeka kwa janga la kibinadamu katika Ukanda wa Gaza kutokana na mvua na baridi kali huko Palestina.
-
OIC: Ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni Ukingo wa Magharibi ni ukiukaji wa sheria za kimataifa
Dec 11, 2025 23:09Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) imelaani mpango mpya wa Wazayuni wa kujenga nyumba 764 katika Ukingo wa Magharibi, ikiitaja hatua hiyo kuwa ni ukiukaji wazi wa sheria za kimataifa na azimio za Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, hasa Azimio nambari 2334.