-
Kwa nini Hamas na makundi ya muqawama ya Palestina yanapinga azimio lililopendekezwa na Marekani?
Nov 17, 2025 07:22Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina (Hamas) imetangaza katika taarifa yake kwamba makundi na harakati za Palestina zimewasilisha waraka kuhusu rasimu ya azimio la Marekani katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na kusisitiza kuwa wamepinga vikali azimio hilo lililopendekezwa na Marekani kupitia waraka huo.
-
Mamdani: Ikiwa Netanyahu atakuja New York katika mkutano ujao wa UNGA nitaamuru akamatwe
Nov 17, 2025 07:19Meya Mteule wa jiji la New York Zohran Kwame Mamdani ameambia televisheni ya ABC News kwamba atatoa hati ya kukamatwa waziri mkuu wa utawala wa kizayuni wa Israel, Benjamin Netanyahu endapo ataingia ndani ya ardhi ya Marekani mwaka ujao kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
-
Mchambuzi: Utawala wa sasa wa Syria utaifanya nchi igawanyike vipande vipande
Nov 17, 2025 07:19Mtafiti wa mahusiano ya kimataifa Yasser Al-Khatib amesema, hali ya mambo nchini Syria ni ngumu na tata mno kutokana na udhaifu wa watawala wake wa sasa, ambao unawasukuma watawala hao kutafuta msaada kutoka nje ya nchi, huku Wasyria wakighariki kwenye dimbwi la mgawanyiko wa nchi unaosababishwa na maslahi yanayokinzana ya nchi zinazoingilia masuala ya ndani ya nchi hiyo.
-
Mahakama ya ICT Bangladesh yamhukumu adhabu ya kifo waziri mkuu wa zamani Hasina
Nov 17, 2025 07:18Baraza la Mahakama la Jinai za Kimataifa (International Crimes Tribunal), ICT la Bangladesh leo limetoa hukumu ya adhabu ya kifo kwa Waziri Mkuu wa zamani aliyeitoroka nchi Sheikh Hasina, baada ya kumpata na hatia ya kuhusika na jinai dhidi ya binadamu-mbali na makosa mengine-, kwa uhalifu uliofanywa mwaka jana wakati wa maandamano makubwa zaidi kuwahi kutokea ya kupinga serikali yake.
-
Kiwanda cha kwanza cha kampuni ya Israel ya uundaji droni za Spike chafunguliwa nchini Morocco
Nov 17, 2025 07:18Kampuni moja ya utawala wa kizayuni wa Israel imefungua kiwanda chake cha kwanza nje ya nchi huko Morocco cha uundaji wa ndege zisizo na rubani za mashambulizi aina ya Spike.
-
Katika kura ya maoni, Waecuador wakataa US kuwa na kituo cha kijeshi tena nchini mwao
Nov 17, 2025 07:17Wananchi wa Ecuador wamekataa pendekezo la kuruhusu kurejeshwa tena nchini humo vituo vya kijeshi vya nchi za kigeni. Hayo ni kwa mujibu wa matokeo ya awali ya kura ya maoni, ambapo hesabu za asilimia 90 ya kura zinaonyesha kuwa karibu theluthi mbili ya walioshiriki wamepiga kura ya “hapana” kupinga pendekezo hilo.
-
Iran yalaani mauaji na ukiukaji wa haki za binadamu unaondelezwa na Israel huko Gaza na Ukingo wa Magharibi
Nov 17, 2025 05:46Iran imelaani vikali mauaji yanayoendelea kufanywa na utawala wa Israel dhidi ya Wapalestina pamoja na ukiukaji wa wazi wa haki za binadamu katika Ukanda wa Gaza na Ukingo wa Magharibi.
-
Afrika Kusini yaanza kufufua miradi ya nyuklia
Nov 17, 2025 05:44Afrika Kusini imeamua kufufua miradi ya nyuklia iliyokwama kwa muda mrefu na kufungua tena vituo muhimu vya utafiti, kama sehemu ya juhudi za kujenga upya utaalamu wa ndani na kujipanga upya katika masoko yanayochipuka ya mafuta ya mitambo ya nyuklia duniani.
-
Ajali ya mgodi yaua watu 32 nchini DRC
Nov 17, 2025 05:43Daraja la mgodi wa kobalti kusini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) limeporomoka na kuua wachimbaji wasiopungua 32, afisa wa serikali ya mkoa alithibitisha Jumapili.
-
Mahitaji ya dhahabu ya Iran yafikia tani 58 Jan–Sep, yashika nafasi ya tano duniani
Nov 17, 2025 05:42Iran imekuwa ni ya tano duniani kwa mahitaji ya dhahabu katika kipindi cha robo tatu za kwanza za mwaka huu, ikichochewa na ongezeko la uagizaji wa dhahabu ili kueneza akiba ya Benki Kuu ya taifa hili.