-
Araqchi: Iran iko tayari kusaidia kutatua mvutano wa mpaka kati ya Pakistan na Afghanistan
Nov 09, 2025 23:48Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, amesema Iran iko tayari kusaidia juhud za kutatua mvutano kati ya Pakistan na Afghanistan ambao umeongezeka hivi karibuni kufuatia mapigano makali ya mpakani.
-
Slovenia: Tunaunga mkono kuanzishwa taifa la Palestina; mauaji ya kimbari yametokea Gaza
Nov 09, 2025 23:48Rais Nataša Pirc Musar wa Slovenia ametangaza kuwa, nchi yake inaunga mkono kuanzishwa kwa taifa la Palestina."
-
Kwa nini China inakosoa hatua za Marekani huko Yemen?
Nov 09, 2025 22:52Sun Lei, naibu mwakilishi wa China katika Umoja wa Mataifa amepinga madai ya mwenzake wa Marekani katika kikao cha Baraza la Usalama na kusisitiza kuwa: Washington imekiuka sheria za kimataifa kwa kuchukua hatua za kijeshi dhidi ya Yemen na kusababisha mateso kwa raia.
-
Iran yapanua diplomasia ya utalii katika mkutano wa Riyadh
Nov 09, 2025 22:52Waziri wa Utalii wa Iran Sayyid Reza Salehi-Amiri jana Jumapili alikutana na kuzungumza kwa nyakati tofauti mjini Riyadh, Saudi Arabia na maafisa wa ngazi ya juu wa nchi kadhaa, wakiwemo maafisa kutoka Indonesia, China, India, Iraq, Tajikistan, Armenia, na Uzbekistan kujadili njia za kupanua ushirikiano wa pande mbili katika sekta ya utalii.
-
Minawi aonya dhidi ya kugawanyika tena Sudan
Nov 09, 2025 22:51Gavana wa Darfur, Minni Arko Minnawi, ameonya kwamba makubaliano yoyote ya kusitisha mapigano nchini Sudan ambayo hayajumuishi ulinzi wa raia na kuwajibishwa wahusika wa uhalifu "yatakuwa na maana ya mgawanyiko wa Sudan," na ametoa wito wa kuondoka wale aliowaita "Janjaweed na mamluki" - akikusudia Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF)- katika maeneo ya makazi ya raia, hospitali na mijini.
-
Magaidi watatu vinara wa al-Shabaab wauawa katika operesheni ya jeshi la Somalia
Nov 09, 2025 22:50Jeshi la Somalia jana Jumapili lilifanya oparesheni kadhaa katika majimbo ya Bakool na Bay na kuuwa wanachama wa ngazi ya juu wa kundi la kigaidi la al Shabaab.
-
Kususia Trump mkutano wa G20; sera za mashinikizo au mshikamano na Israel?
Nov 09, 2025 09:30Rais wa Marekani alitangaza kuwa, hakuna maafisa wa Marekani watakaohudhuria mkutano wa kila mwaka wa Kundi la G20 huko Johannesburg, Afrika Kusini.
-
Qalibaf: Marekani lazima ikubali matokeo ya uchokozi wake wa wazi dhidi ya Iran
Nov 09, 2025 08:20Spika wa Bunge la Iran, Mohammad Baqer Qalibaf, anasema Marekani lazima ikabiliane na matokeo ya kisheria na kisiasa ya kitendo chake cha uchokozi mbaya dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu, mapema mwaka huu.
-
Afisa wa Yemen: Mtandao wa ujasusi wa Marekani, Israel na Saudi Arabia unataka kukomesha himaya ya Yemen kwa Palestina
Nov 09, 2025 08:19Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Kisiasa la Yemen amevipongeza vikosi vya usalama vya nchi hiyo kwa kuvunja mtandao wa ujasusi uliounganishwa na mashirika ya ujasusi ya Marekani, Israel na Saudi Arabia, akisema kuwa kundi hilo la ujasusi lilitaka zaidi kupunguza uungaji mkono na himaya ya serikali ya Sana'a kwa Palestina.
-
Rais wa Colombia amshambulia Trump: Wewe na marafiki zako ni waongo
Nov 09, 2025 06:59Rais wa Colombia, Gustavo Petro, amemshambulia Rais wa Marekani, Donald Trump, akionya kwamba kinachoendelea huko Gaza kinaweza pia kutokea Kusini mwa Dunia.