-
Mtandao wa Madaktari Sudan: RSF imeteketeza mamia ya miili ya watu huko El Fasher
Nov 09, 2025 06:34Mtandao wa Madaktari wa Sudan umesema kwamba Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) vilikusanya mamia ya miili kutoka mitaani na vitongoji vya makazi ya raia vya El Fasher (mji mkuu wa Darfur Kaskazini) na kuzika baadhi ya miili hiyo katika makaburi ya umati, huku mingine ikichomwa moto kabisa.
-
Mamia watoweka baada ya boti kuzama katika mpaka wa Malaysia na Thailand
Nov 09, 2025 05:56Mamlaka ya Usafiri wa Baharini ya Malaysia imetangaza kwamba takriban watu 290 bado hawajulikani walipo leo Jumapili baada ya boti iliyokuwa imebeba watu wapatao 300 kuzama karibu na mpaka wa Malaysia na Thailand, huku manusura 10 wakiokolewa na mwili mmoja kupatikana.
-
Russia yaimarisha maandalizi ya vita ya nyuklia kufuatia maagizo ya Rais Putin
Nov 09, 2025 04:07Wizara ya mambo ya nje ya Russia imeanza kuchukua hatua za kutathmini uwezo wa taifa katika nyanja za nyuklia, kufuatia maagizo ya Rais Vladimir Putin wa nchi hiyo. Hayo ni kwa mujibu wa taarifa ya Waziri wa Mambo ya Nje, Sergei Lavrov.
-
Israel yaua watu watatu Kusini mwa Lebanon baada ya kutishia mashambulizi mapya ya kijeshi
Nov 09, 2025 04:01Jeshi la Israel limewaua watu watatu katika maeneo ya kusini mwa Lebanon kupitia mashambulizi ya anga yaliyotekelezwa kwa nyakati tofauti, siku chache tu baada ya kutoa onyo la kuanzisha mashambulizi makubwa dhidi ya taifa hilo jirani.
-
Maandamano Paris kulaani mauaji ya halaiki Sudan, UAE yashutumiwa kwa kuunga mkono RSF
Nov 09, 2025 03:56Mamia ya waandamanaji walikusanyika Jumamosi karibu na Mnara maarufu wa Eiffel mjini Paris kulaani mauaji ya halaiki yanayoendelea nchini Sudan, huku wakiishutumu serikali ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) kwa kuwafadhili na kuwapatia silaha waasi wa RSF wanaotekeleza mauaji ya raia.
-
Iraq yaanza upigaji kura maalum wa uchaguzi wa bunge kwa wanajeshi na wakimbizi
Nov 09, 2025 03:50Mchakato wa upigaji kura maalum kwa ajili ya wanajeshi na wakimbizi katika uchaguzi wa bunge la Iraq umeanza rasmi leo Jumapili katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo.
-
Maandamano yazuka Nigeria kufuatia tishio la Trump la kuivamia nchi hiyo kijeshi
Nov 09, 2025 03:48Wananchi walimiminika mitaani siku ya Jumamosi katika jiji la Kano, kaskazini mwa Nigeria, kupinga vitisho vya Rais Donald Trump wa Marekani, vya kuivamia nchi hiyo kijeshi.
-
Iran iko tayari kwa mchakato wa kuzalisha ndege za abiria ilizojibunia yenyewe
Nov 09, 2025 00:00Mkuu wa Shirika la Usafiri wa Anga la Iran amesema kuwa, baada ya kubuni na kutengeneza ndege ya mizigo, sasa wataalamu wa Iran wako katika mchakato wa kubuni na kuzalisha kwa wingi ndege za abiria.
-
Palestina: Hati zilizotolewa na Uturuki za kukamatwa viongozi wa Israel ni 'ushindi kwa haki'
Nov 08, 2025 23:59Palestina imesifu na kupongeza hatua ya Uturuki ya kutoa hati za kukamatwa viongozi 37 wa utawala wa kizayuni wa Israel na kuielezea kuwa ni 'ushindi kwa haki' huku ikizitolea mwito nchi zingine kufuata mfano wa Ankara.
-
Zawadi ya dola trilioni moja kwa Musk mkabala wa njaa inayowakabili Wamarekani milioni 42; Uadilifu au mkanganyiko?
Nov 08, 2025 23:20Huku mamilioni ya Wamarekani wakihangaika kumudu milo yao ya kila siku, wanahisa wa Kampuni ya Tesla wamepasisha kifurushi cha fidia ambacho hakijawahi kushuhudiwa cha dola trilioni moja kwa Elon Musk. Tofauti na kukinzana huku kukubwa kati ya utajiri wa mtu mmoja na umaskini uliokithiri wa mamilioni ya watu kumefichua taswira halisi ya pengo la pato nchini Marekani.