-
Rais Pezeshkian: Mazishi ya Kiongozi wa Iran ni kielelezo cha umoja wa kitaifa
Jul 09, 2026 03:33Rais Masoud Pezeshkian amesema mahudhurio makubwa ya watu kutoka matabaka yote ya jamii katika mazishi makubwa yaliyofanyika kwa ajili ya Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, ni kielelezo cha umoja wa kitaifa nchini Iran.
-
Pezeshkian: Unyanyasaji wa Marekani katika Kombe la Dunia unaakisi sera ya kigeni ya Washington
Jul 09, 2026 03:30Rais wa Iran Masoud Pezeshkian amesema Marekani imegeuza Kombe la Dunia FIFA la 2026 kuwa uwanja mwingine wa uonevu na mashinikizo ya kisiasa, akisisitiza kuwa mwenendo wa Washington kama mwenyeji wa michezo hiyo unaonyesha sera zile zile inazotekeleza kote duniani.
-
Spika wa Bunge la Iran: Zama za uonevu wa Marekani zimekwisha
Jul 09, 2026 03:26Spika wa Bunge la Iran, Mohammad Baqer Qalibaf, ameikosoa Marekani kwa kukiuka Mkataba wa Maelewano kati ya Iran na Marekani (MoU), akisisitiza kwamba "zama za uonevu na ulaghai" wa Washington zimekwisha.
-
Kambi ya kijeshi inayofadhiliwa na UAE yaanza kuonekana katika eneo la Berbera huko Somaliland
Jul 09, 2026 03:22Picha za satalaiti zilizochambuliwa na Le Monde zinaonyesha kuwa kambi ya kijeshi inayofadhiliwa na Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) inajengwa huko Berbera, Somaliland, karibu na Lango-Bahari la Bab al-Mandeb.
-
Human Rights Watch yatahadharisha kuhusu kukandamizwa wapinzani Tunisia
Jul 09, 2026 03:04Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Human Rights Watch (HRW) limelaani kile ilichokitaja kuwa ni ukandamizaji unaofanywa na mamlaka husika nchini Tunisia kwa wapinzani wa kisiasa na wanaharakati wa haki za binadamu.
-
Mamilioni wamuaga Kiongozi Shahidi Ayatullah Khamenei katika miji ya Najaf na Karbala nchini Iraq
Jul 08, 2026 14:19Mamilioni ya waombolezaji leo Jumatano walikusanyika katika miji mitakatifu ya Najaf na Karbala nchini Iraq kwa ajili ya kuaga na kutoa heshima zao za mwisho kwa Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei na familia yake waliouliwa shahidi katika mashambulizi ya Marekani na Israel dhidi ya Iran.
-
Kamanda wa Jeshi la Wanamaji: Fukwe za Iran zitakuwa jehanamu kwa jeshi lolote vamizi
Jul 08, 2026 14:15Admeri Habibullah Sayyari Naibu Mratibu wa Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa jaribio lolote la majeshi ya kigeni kutua katika pwani ya Iran litakabiliwa na jibu kali sana, na kuonya kuwa ukanda wa pwani ya Iran utageuka kuwa "jehanamu" kwa jeshi lolote vamizi.
-
Iran: Chanzo cha uungaji mkono wowote kwa jeshi Marekani ni shabaha halali
Jul 08, 2026 14:10Makao Makuu ya Majeshi ya Iran, Khatamul-Anbiya (SAW) yametangaza kuwa chanzo chochote cha uungaji mkono unaotolewa kwa "jeshi vamizi la Marekani" katika mashambulizi dhidi ya mamlaka ya kujitawala na ardhi nzima ya Iran ni shabaha halali ya vikosi vya ulinzi.
-
Shambulio la droni la RSF lauwa raia 10 waliokuwa wakielekea harusini katikati mwa Sudan
Jul 08, 2026 12:20Mtandao wa Madaktari wa Sudan leo umeripoti kuwa shambulio la ndege zisizo na rubani lililofanywa na wanamgambo wa Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) limeua raia 10, wakiwemo wanawake watano kutoka familia moja, katikati mwa Sudan walipokuwa wakieleke harusini.
-
Rais wa Zimbabwe asaini sheria ya kuongeza muda wa kubaki madarakani kwa miaka 2 zaidi
Jul 08, 2026 12:15Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe ametia saini marekebisho ya katiba yanayoongeza muda wake wa kusalia madarakani hadi mwaka 2030.