-
Mkuu wa Majeshi ya Uganda aamuru kufungwa NTV Uganda na vyombo vingine vya habari
Jun 28, 2026 09:12Mkuu wa Majeshi ya Uganda, Jenerali Muhoozi Kainerugaba ametoa amri ya kufungwa televisheni ya NTV na vyombo vingine vya habari.
-
Jeshi la Iran lalenga vituo vya jeshi la Marekani kujibu uchokozi
Jun 28, 2026 04:34Jeshi la Iran la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limetangaza kuwa limeendesha oparesheni kubwa ya makombora na ndege zisizo na rubani (droni) dhidi ya vituo nane vya kijeshi vya Marekani katika kanda hii, likiitaja hatua hiyo kuwa “jibu madhubuti” dhidi ya uchokozi mpya wa Marekani kwenye ardhi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
-
DRC yaishtaki Rwanda ICJ kwa tuhuma za unyanyasaji
Jun 28, 2026 04:32Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imewasilisha kesi dhidi ya Rwanda katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki ICJ, ikiituhumu nchi hiyo jirani kwa vitendo vya ukatili katika eneo lenye utajiri wa madini la mashariki mwa DRC.
-
Volker Turk aonya kuongezeka vifo vya wahamiaji katika utawala wa Trump
Jun 28, 2026 04:30Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Türk imetoa taarifa na kuonyesha wasiwasi kuhusu ongezeko kubwa la vifo vya wahamiaji vinavyotokea katika vituo vya kuwazuilia wahamiaji nchini Marekani wakati wa muhula wa pili wa utawala wa Donald Trump, na ametaka kufanyika uchunguzi huru kuhusu suala hilo.
-
Meja Jenerali Rezaei: Kama adui ataanzisha vita vingine, atapata maafa na hasara kubwa
Jun 28, 2026 04:29Kamanda wa zamani wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amesema, "Iwapo adui atafanya kosa na kuanzisha vita vipya, vita hivyo havitakuwa tena kama vita vya tatu vya kulazimishwa, bali vitasababisha hasara na maafa makubwa ya kibinadamu.
-
Ireland: Wanamichezo waungana kupinga uhusiano wa kimichezo na utawala wa Kizayuni
Jun 28, 2026 04:24Mji mkuu wa Ireland, Dublin, umeshuhudia kufanyika kwa wakati mmoja shughuli mbalimbali za wananchi na matukio ya michezo yaliyolenga kuunga mkono Palestina na kupinga kuanzishwa uhusiano wa kimichezo na utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Araqchi azungumzia makubaliano ya Islamabad na mawaziri wenzake wa mambo ya nje
Jun 27, 2026 11:09Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araqchi, amefanya mfululizo wa mazungumzo kwa njia ya simu na mawaziri wa kutoka Pakistan, Misri, Falme za Kiarabu (UAE), Uingereza, na Romania, ambapo walijadili makubaliano ya Islamabad pamoja na maendeleo ya karibuni katika ukanda.
-
Iran yakemea hujuma ya Marekani kusini mwa nchi, yaitaja kuwa “ukiukaji wa wazi” wa MoU ya Islamabad
Jun 27, 2026 11:07Iran imekemea mashambulizi ya hivi karibuni ya anga ya Marekani dhidi ya maeneo kadhaa kando ya pwani za kusini mwa nchi, ikiyataja kuwa “ukiukaji wa wazi” wa hati ya makubaliano ya maelewano (MoU) iliyopatanishwa na Pakistan.
-
Maandamano kote Lebanon kupinga makubaliano yanayoungwa mkono na Marekani na Israel
Jun 27, 2026 11:04Maelfu ya wananchi wa Lebanon wamejitokeza mitaani katika miji na maeneo mbalimbali kupinga “makubaliano” yanayoungwa mkono na Marekani kati ya Lebanon na utawala wa Israel, huku wakiyataja kuwa tishio kwa mamlaka ya taifa lao.
-
Mlipuko wa Ebola waongeza mateso kwa wananchi wa mashariki mwa DRC
Jun 27, 2026 10:55Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wamejulishwa kuwa kuongezeka kwa mapigano, kuzorota kwa hali ya kibinadamu na mlipuko mpya wa Ebola kunazidi kuongeza mateso kwa wananchi wa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, (DRC) licha ya juhudi za kikanda za kuleta amani kuendelea kupata mafanikio.