-
IOM: Hali mbaya ya usalama imelazimisha mamia ya Wasudan kuhama makazi yao Kordofan Kusini
Jan 30, 2026 04:15Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji (IOM) limetangaza kuwa watu wasiopungua 285 ni miongoni mwa wale waliolazimika kuyahama makazi yao kwenye kipindi cha siku mbili za karibuni katika miji ya Kadugli na Al-Kuwaik iliyoko kwenye Jimbo la Kordofan Kusini nchini Sudan kutokana na hali mbaya ya usalama.
-
Araqchi: Vikosi vya Jeshi la Iran vinashikilia kitufe cha kufyatua risasi
Jan 29, 2026 23:43Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Sayyid Abbas Araqchi, ameandika kwenye chaneli ya X, akijibu vitisho vya hivi karibuni vya Rais Donald Trump wa Marekani kwamba: "Vikosi vyetu vya jeshi vimeshikilia kitufe cha kufyatua risasi na viko tayari kujibu haraka na kwa kina uchokozi wowote dhidi ya ardhi, anga na maji ya nchi hii."
-
Qalibaf: Iran haipingi mazungumzo, inataka diplomasia ichukue mkondo wake
Jan 29, 2026 23:42Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge) amesema kuwa Tehran haipingi msingi wa mazungumzo na diplomasia ambao lazima uwe wa aina yake na wenye mlingano kwa mujibu wa kuheshimiana pande mbili.
-
Guterres ataja vipaumbele vyake katika mwaka wake wa mwisho kama Katibu Mkuu wa UN
Jan 29, 2026 23:42Katika wakati ambapo mivutano ya kimataifa inaongezeka huku hatua zisizo na tahadhari zikisababisha madhara hatari, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametoa wito wa kuimarishwa juhudi za amani, haki na maendeleo endelevu.
-
Somalia yamteua mkuu mpya wa jeshi kuchukua nafasi ya Jenerali Rage
Jan 29, 2026 23:19Baraza la Mawaziri la Somalia limemteua Brigedia Jenerali Ibrahim Mohamed Mohamud kuwa Kamanda mpya wa Jeshi la Taifa la Somalia (SNA). Hii ni kwa mujibu wa taarifa rasmi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu wa Somalia iliyosomwa na msemaji wa serikali, Abdinasir Ahmed Bashir.
-
Shirika la Ndege la Ethiopian Airlines limefuta safari zake kwenda Tigray kwa sababu ya mapigano
Jan 29, 2026 23:18Shirika la ndege la Ethiopian Airlines limefuta safari za ndege kuelekea kaskazini mwa mkoa wa Tigray baada ya mapigano ya silaha kuzua hofu ya kuibuka mzozo mpya katika eneo hilo.
-
Iran na Saudia katika mkondo wa ushirikiano na matarajio ya kuleta usalama, ustawi na umoja baina ya Waislamu
Jan 29, 2026 23:17Rais Masoud Pezeshkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, amefanya mazungumzo kwa njia ya simu na mrithi wa Ufalme wa Saudi Arabia, Mohammed Bin Salman na kusisitiza kwamba: muelekeo inaofuata Iran katika uga wa kikanda umejengwa juu ya msingi wa udugu wa Kiislamu, kustawisha uhusiano wa kirafiki, na kupanua mashirikiano na nchi za Kiislamu.
-
Droni 1,000 za kimkakati zakabidhiwa kwa Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran
Jan 29, 2026 09:55Ndege elfu moja zisizo na rubani za kimkakati zimejiunga na vikosi vinne vya jeshi kwa amri ya Meja Jenerali Amir Hatami, Kamanda Mkuu wa Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
-
'Ni rahisi - Trump ameshindwa': Wanamtandao wakosoa vitisho vya kijeshi vya Marekani dhidi ya Iran
Jan 29, 2026 09:35Watumiaji wa mitandao ya kijamii wamekosoa vitisho vya kijeshi vya mara kwa mara vya Rais wa Marekani, Donald Trump dhidi ya Iran, ambapo hivi karibuni alitishia Iran kwa kisingizio cha miradi ya nyuklia ya nchi hiyo. Wamesema kuwa Israel inaiburuta Washington katika vita vingine kwa niaba ya serikali ya Tel Aviv.
-
China yaitahadharisha Marekani kuhusu vita dhidi ya Iran
Jan 29, 2026 09:16China imetahadharisha kwamba hatua hatari za kijeshi zinazoongozwa na Marekani dhidi ya Iran zinaweza kuyumbisha eneo la magharibi mwa Asia na kuisukuma kanda hiyo kwenye matokeo yasiyotabirika.