-
Juhudi za uokoaji zinaendelea Msumbiji baada ya wiki kadhaa za mvua kubwa
Jan 29, 2026 09:10Juhudi za utafutaji na uokoaji zinaendelea kufanywa nchini Msumbiji baada ya wiki kadhaa za mvua kubwa iliyosababisha mafuriko makubwa, kuzamisha ardhi ya mashamba, kubomoa nyumba na miundombinu kujaa maji.
-
Milio ya risasi yasikika mapema leo karibu na uwanja wa ndege wa mji mkuu wa Niger
Jan 29, 2026 09:03Milio ya risasi ilisikika mapema leo karibu na uwanja wa ndege wa kimataifa katika mji mkuu wa Niger, Niamey kabla ya hali ya utulivu kurejea.
-
IRGC: Iran haitaanzisha vita, lakini ndiyo itakayoamua vitakavyoisha
Jan 29, 2026 03:49Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limesema Iran ndiyo inayoshikilia mpini na nafasi ya juu katika kuamua hatima ya vita vyovyote tarajiwa, likisisitiza kwamba kutumia mashinikizo ya kijeshi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu hakujazaa matunda.
-
Sababu zilizomfanya Katibu Mkuu wa UN akiri kuwa 'Sheria ya Msituni' ndiyo inayotawala hivi sasa duniani
Jan 29, 2026 03:30Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amekiri kuwa sheria ya msituni ndiyo inayotawala hivi sasa duniani na kusisitiza kwamba kuna udharura wa kufanyika mageuzi katika Baraza la Usalama la umoja huo.
-
Waislamu Canada wataka kukomeshwa chuki dhidi ya Uislamu
Jan 29, 2026 03:06Viongozi wa Waislamu nchini Canada wametoa wito wa kukomeshwa kwa matamshi ya chuki na uenezaji wa hofu dhidi ya Uislamu na Waislamu, huku nchi hiyo ikijiandaa kuadhimisha miaka tisa tangu kutokea shambulio baya dhidi ya msikiti katika mkoa wa Quebec.
-
Nujaba kwa maadui wa Iran: Vita vinaweza kufika milangoni kwenu
Jan 29, 2026 02:57Katibu Mkuu wa kundi la kupambana na ugaidi la Harakat al-Nujaba la Iraq amewaonya vikali maadui wa Iran kuhusu matokeo mabaya ya uchokozi wowote mpya ambao wanaweza kufanya dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu.
-
ECOWAS pia yatangaza kuiondolea vikwazo Guinea
Jan 29, 2026 02:35Jumuiya ya Kiuchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi (ECOWAS) imetangaza kuondoa vikwazo vyote vilivyobaki ilivyowekea Guinea kufuatia mapinduzi ya kijeshi ya mwaka 2021.
-
Utafiti: UK inaendelea kusakamwa na uchochole
Jan 29, 2026 02:35Umaskini nchini Uingereza umezidi kuwa mbaya, huku idadi kubwa ya watu wakiishi katika hali ngumu wasiweze kumudu mahitaji yao ya msingi, hayo ni kwa mujibu utafiti uliofanywa na shirika moja la kutoa misaada.
-
Araghchi: Mazungumzo hayawezi kufanikiwa chini ya vitisho
Jan 29, 2026 00:19Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Sayyid Abbas Araghchi ameonya kwamba, kutwisha diplomasia kupitia vitisho vya kijeshi hakuwezi kuwa na ufanisi au tija, akisema kwamba hakuna uamuzi wowote ambao umefanywa na Tehran kufikia juu ya kufanya mazungumzo na Marekani.
-
Iran: Maadui wajiandae kwa 'jibu la uharibifu' wakituchokoza
Jan 29, 2026 00:18Kamanda mwandamizi wa Jeshi la Iran ameonya kwamba, hatua yoyote ghalati dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu itawasababishia maadui uharibifu mkubwa, akisisitiza kwamba vitisho dhidi ya Tehran kupitia maonyesho ya kijeshi havilishughulisha taifa hili.