Mar 14, 2024 02:34 UTC
  • Maandamano ya kuiunga mkono Palestina karibu na ubalozi wa utawala wa Kizayuni Jordan

Maandamano ya kuinga mkono Palestina yamefanyika karibu na ubalozi wa utawala wa Kizayuni huko Amman mji mkuu wa Jordan.

Mamia ya wananchi wa Jordan wakazi wa mji mkuu wa nchi hiyo wameandamana karibu na ubalozi wa utawala wa Israel huko Amman kuiunga mkono Palestina. Waandamanaji walikuwa wakipiga nara" tunajitolea nafsi na roho zetu kwa ajili ya Palestina, na " Ukanda wa Gaza hauko peke yake; "Wajordani wote wako pamoja na Hamas."  

Yanal Freihat, mjumbe wa bunge la Jordan, amewaambia waandishi wa habari: Washiriki katika maandamano ya jana wawametaga utiifu wao kwa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina  (Hamas) na brigedi zote za muqawama huko Ukanda wa Gaza, na kwamba wananchi wote wa Jordan  wako pamoja na muqawama wa Palestina.  

Yanal Freihat, mbunge wa Jordan 

 

Wakati huo huo Ahmad al Rami Msemaji wa Muungano dhidi ya utawala wa Kizayuni huko Jordan pia amesema kuwa: Leo hii tumefikka hapa kwa lengo la kuuunga mkono mapambano ya ukombozi katika Ukanda wa Gaza na wananchi wote wa Palestina."  

Jinai zinazoendea kufanywa na utawala wa Israel unaotekeleza mauaji ya kimbari dhidi ya raia wa Ukanda wa Gaza zimekabiliwa na radiamali mbalimbali katika pembe mbalimbali za dunia ambapo wananchi katika nchi mbalimbali, serikali na taasisi za kimataifa wanaendelea kufanya maandamano ya kulaani mauaji ya kimbari dhidi ya wakazi wa Ukanda na kuwaunga mkono wananchi madhulumu wa Palestina.  

 

Tags