Apr 17, 2024 02:57 UTC
  • UN: Israel imeua wanawake 10,000 Gaza

Takriban wanawake 10,000 wameuawa huko Gaza tangu utawala haramu wa Israel uanzishe vita vya mauaji ya kimbari dhidi ya eneo hilo Oktoba mwaka jana.

Hayo yamedokezwa na  Shirika la Umoja wa Mataifa linalihusika na masuala ya wanawake UN Women katika ripoti yake mpya ambayo imeeleza kuwa: “Katika miezi sita ya vita, wanawake 10,000 wa Kipalestina huko Gaza wameuawa, kati yao akina mama wanakadiriwa kuwa 6,000, wakiwaacha watoto 19,000 yatima.”

Aidha ripoti hiyo imesema hivi sasa mtoto mmoja anajeruhiwa au kuuawa kila baada ya dakika 10 katika Ukanda wa Gaza.

Nalo shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya Afya WHO limetoa wito mpya wa kusitisha mapigano ili misaada ya kibinadamu iweze kupelekwa Gaza kusaidia kujenga upya hospitali ikiwemo ya Al Shifa, ambayo "kimsingi imeharibiwa" baada ya uvamizi wa Israel hivi karibuni.

Israel ilianzisha vita dhidi ya Gaza Oktoba 7 baada ya operesheni ya kulipiza kisasi ya wapigani ukombozi wa Palestina na hadi sasa jeshi katilila Israel limeua takriban Wapalestina 33,800, wengi wao wakiwa wanawake na watoto na wengine 76,500 kujeruhiwa huku kukiwa na uharibifu mkubwa na uhaba wa mahitaji.