Apr 18, 2024 04:28 UTC
  • Utawala wa Kizayuni wazidi kutengwa kimataifa

Gazeti la Kizayuni la Haaretz limeandika katika ripoti yake kuwa Israel inaendelea kutengwa pakubwa duniani kote.

Haaretz limesisitiza namna utawala wa Kizayuni wa Israel unavyozidi kutengwa na kuandika kuwa: Israel inazidi kutengwa kimataifa na iwapo utawala huo hautabadili kikamilifu siasa zake na kuleta mabadiliko katika sera zake kutengwa huko kutaendelea kushuhudiwa.  

Uzi Baram, Waziri wa Mambo ya Ndani na mjumbe wa zamani wa Knesset (Bunge la utawala wa Kizayuni) pia ameandika katika makala moja kwenye  gazeti la Haaretz kwamba Israel, Marekani na baadhi ya nchi waitifaki wao zinashrikiana wakati tu wa migogoro ya kimataifa; na ushirikiano huo si wa kudumu.

Kuhusiana na suala hilo, gazeti hilo la Kizayuni limeendelea kuandika kuwa: Israel haiwezi kujidanganya kwamba inaweza kutegemea ushirikiano huo siku zote. 

Wizara ya Afya ya Palestina imetangaza kuwa, hadi sasa Wapalestina karibu elfu 34 wameuliwa shahidi wengi wao wakiwa ni wanawake na watoto tangu utawala wa Kizayuni uanzishe vita jinai za kutisha dhidi ya wakazi wa Ukanda wa Gaza Oktoba 7 mwaka jana. 

Mauaji ya kimbari ya utawala wa Kizayuni dhidi ya wakazi wa Gaza 

 

Tags