-
Makumi wapoteza maisha wakigombania 'mafuta ya upako' Tanzania + Sauti
Feb 02, 2020 00:13Kwa akali watu 20 wameaga dunia katika mkanyagano wa harakati za kutaka kukanyaga 'mafuta ya upako' kwenye kongamano la 'Mtume' Boniface Mwaiposa lililofanyika uwanja wa Majengo mjini Moshi mkoani Kilimanjaro, kaskazini mashariki mwa Tanzania jioni ya jana Jumamosi.
-
Waislamu Kenya waadhimisha Siku ya Vazi la Hijab Duniani + Sauti
Feb 01, 2020 12:17Vyama vya Kiislamu nchini Kenya vimehimizwa kushadidisha hamasa juu ya vazi la hijab miongoni mwa Waislamu kama njia pekee ya kukinusuru kizazi cha Kiislamu dhidi ya sheria dhalimu zinazomkandamiza binti wa Kiislamu. Mwito huo umetolewa sanjari na maadhimisho ya Siku ya Vazi la Hijab Duniani ambayo huadhimishwa Februari Mosi kila mwaka. Seifullah Muurtadha na maelezo zaidi kutoka Mombasa, Kenya.
-
SAUTI, Shirika la Msalaba Mwekundu lawataka wahisani duniani kutuma misaada yao ili kuwasaidia waathirika wa mapigano ya hivi karibuni
Jan 29, 2020 12:37Shirika la Msalaba Mwekundu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati limewataka wahisani duniani kutuma misaada yao kwenda shirika hilo ili liweze kuwahudumia watu walioathirika na mapigano ya hivi karibuni nchini humo.
-
Wahalifu wanaotafuta damu ya watoto 1000 kufanya kafara Gabon wamekuwa janga + Sauti
Jan 27, 2020 23:00Wazazi katika mji mkuu wa Gabon, Libreville, Jumatatu, Januari 27, 2020 hawakuwaruhusu watoto wao kwenda skuli licha ya serikali kuweka ulinzi mkali katika skuli zote za mji huo mkuu. Wazazi hao wanasema kuwa hatua hiyo pekee haiwezi kuwazuia wahalifu wanaotafuta damu za watoto elfu moja kama kafara ya kuwabakisha madarakani. Mossi Mwasi na maelezo zaidi kutoka Brazzaville.
-
Chama cha FDC chailaumu vikali serikali ya Uganda + Sauti
Jan 20, 2020 12:48Kwa mara nyingine tena, mwanasiasa mkongwe katika chama cha FDC nchini Uganda, Daktari Kizza Besigye ameikosoa vikali serikali ya Rais Yoweri Museveni kutokana na ubabe na ukandamizaji unaofanywa na vyombo vya dola dhidi ya wapinzani. Kigozi Ismail na maelezo zaidi kutoka Kampala.
-
Wazanzibar: Miaka 56 baadaye, malengo ya Mapinduzi hayajafikiwa
Jan 12, 2020 13:14Sherehe za maadhimisho ya miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar zimefanyika leo Jumapili katika Uwanja wa Abeid Aman Karume kisiwani Unguja.
-
Zarif: Iran imeshambulia kambi za Marekani nchini Iraq kwa mujibu wa kifungu cha 51 cha UN cha haki ya kujilinda + Video
Jan 08, 2020 07:11Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amezungumzia hatua iliyochukuliwa leo na Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH ya kuwashambulia magaidi wa Kimarekani katika kambi ya kijeshi ya Ain al Asad nchini Iraq na kusisitiza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetoa jibu hilo kali kwa kutegemea kifungu nambari 51 cha Hati ya Umoja wa Mataifa cha haki ya kujilinda.
-
Wakazi wa kaskazini mwa Bujumbura waendelea kuteseka kwa madhara ya mafuriko + Sauti
Jan 07, 2020 05:01Waathiriwa wa mafuriko katika baadhi ya maeneo ya kaskazini mwa Bujumbura waliopiga kambi katika madarasa ya shule wametakiwa kuondoka ili kuruhusu sehemu ya pili ya mwaka wa shule kuanza. Hata hivyo raia hao wanalalamika kutokuwa na sehemu ya kwenda. Hali hiyo imepelekea baadhi ya shule katika eneo hilo kuakhirisha kufungua muhula mpya wa masomo. Hamida Issa na maelezo zaidi kutoka Bujumbura…
-
Kiongozi Muadhamu asalisha Sala ya Maiti ya Luteni Jenerali Soleimani na mashahidi wenzake + Video
Jan 06, 2020 04:46Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu leo asubuhi amesalisha Sala ya Maiti ya Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH na mashahidi wenzake waliouliwa kigaidi na Marekani nchini Iraq, usiku wa kuamkia Ijumaa ya tarehe 3 Januari 2020.
-
Ismail Hania ametoka Ghaza kuja Tehran kushiriki maziko ya Kamanda Soleimani; asema Soleimani ni shahidi wa Quds + Video
Jan 06, 2020 04:43Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS ametilia mkazo wajibu wa kuendelea na muqawama hadi ardhi zote za Palestina zitakapokombolewa.