Klabu Bingwa Ulaya: Arsenal yainyuka 2-0 Basel, Walcott ang'ara
https://parstoday.ir/sw/news/uncategorised-i16315-klabu_bingwa_ulaya_arsenal_yainyuka_2_0_basel_walcott_ang'ara
Michuano ya klabu bingwa barani Ulaya imeendelea katika hatua ya makundi ambapo usiku wa kuamkia leo viwanja vinane vilikuwa msambweni wakati klabu za makundi mbalimbali zilipokutana kuwania pointi tatu muhimu.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Sep 29, 2016 04:43 UTC
  • Klabu Bingwa Ulaya: Arsenal yainyuka 2-0 Basel, Walcott ang'ara

Michuano ya klabu bingwa barani Ulaya imeendelea katika hatua ya makundi ambapo usiku wa kuamkia leo viwanja vinane vilikuwa msambweni wakati klabu za makundi mbalimbali zilipokutana kuwania pointi tatu muhimu.

Wabeba Bunduki wa London Arsenal ya Uingereza wakiwa nyumbani walibuka na ushindi wa  mabao 2 kwa nunge dhidi ya Basel ya ya Uswisi huku magoli yote yakiwekwa kimiani na winga machachari Theo Walcott.

PSG ya Ufaransa ikiwa ugenini iliibuka na ushindi mnono wa 3-1 dhidi ya Ludogorets Razgrad ya nchini Bulgaria.

Besiktas imeenda sare ya 1-1 dhidi ya Dynamo Kyiv. Huku SSC Napoli ikiibuka na ushindi wa 4-2 dhidi ya Benfica.

Wachezaji wa Celtic wakishangilia baada ya kufunga bao

Borussia Moenchengladbach nayo ikiwa nyumbi imekubali kichapo cha 2-1 kutoka kwa Barcelona ya Uhispania. Na mchezo wa kushangaza wa funga nikufunge ulikuwa kati ya Celtic na Manchester City, ambapo  timu hizo zilienda sare ya kufungana mabao 3-3.

Atletico Madrid nayo ikiwa nyumbani ilifanya kazi kubwa baada ya kuibuka na ushindi  wa 1-0 dhidi ya Bayern Munich. Vijana hao wa Madrid wangeweza kupata ushindi mnono lakini walikosa penalty. Na FC Rostov ikiwa nyumbani ililazimishwa sare ya 2-2 na timu ya  PSV Eindhoven.