Gesi zaidi yagunduliwa katika pwani ya Tanzania
https://parstoday.ir/sw/news/uncategorised-i1975-gesi_zaidi_yagunduliwa_katika_pwani_ya_tanzania
Tanzania imegundua takribani futi za ujazo trillioni 2.17 za Gesi katika eneo la Ruvu lililoko katika Mkoa wa Pwani kilomita chache kutoka katika jiji la Dar es Salaam.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 26, 2016 04:21 UTC
  • Gesi zaidi yagunduliwa katika pwani ya Tanzania

Tanzania imegundua takribani futi za ujazo trillioni 2.17 za Gesi katika eneo la Ruvu lililoko katika Mkoa wa Pwani kilomita chache kutoka katika jiji la Dar es Salaam.

Taarifa zaidi zinasema kuwa, huu ni ugunduzi mkubwa zaidi wa gesi pembezoni mwa ufukwe wa bahari ya Hindi. Badra Masoud, Msemaji wa Wizara ya Nishati na Madini nchini Tanzania amesema kuwa, gesi hiyo iliyogunduliwa ina thamani ya takribani shilingi za Kitanzania trillioni 12 sawa na takribani dola za Kimarekani bilioni 6. Tanzania bado inaamini huenda kuna gesi zaidi itagunduliwa kwa kuwa utafiti zaidi bado unaendelea. Msemaji wa Wizara ya Nishati na Madini nchini Tanzania, uvunaji wa gesi hii utaanza muda wowote mara tu baada ya kukamilika kwa miundombinu ambapo gesi nyingine itauzwa nje na nyingine itaifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda.

Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akiongea na wanahabari amedokeza kuwa baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam tayari wameshaanza kunufaika moja kwa moja na gesi ambayo iligunduliwa katika maeneo mengine huko mkoani Mtwara na Lindi.

Kwa mujibu wa Waziri Muhongo, Tanzania imetenga kiasi cha takribani dola milioni 6 za Kimarekani za kufanyia tathmini na kuwalipa watu watakaokutwa katika eneo ambalo kutajengwa mtambo mkubwa wa gesi katika mkoa wa Lindi.