Kuongezeka marufuku ya uhuru wa kutoa maoni nchini Saudi Arabia
https://parstoday.ir/sw/news/uncategorised-i358-kuongezeka_marufuku_ya_uhuru_wa_kutoa_maoni_nchini_saudi_arabia
Wizara ya Masuala ya Kiislamu na Miongozo nchini Saudi Arabia imetangaza kupiga marufuku kikamilifu uhuru wa kujieleza na kutoa maoni na imekwenda mbali zaidi na kusema kuwa, ni marufuku kwa Maimamu wa Misikiti kutoa hotuba au kufanya kikao misikiti pasina kupata kibali cha serikali.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 01, 2016 03:17 UTC
  • Kuongezeka marufuku ya uhuru wa kutoa maoni nchini Saudi Arabia

Wizara ya Masuala ya Kiislamu na Miongozo nchini Saudi Arabia imetangaza kupiga marufuku kikamilifu uhuru wa kujieleza na kutoa maoni na imekwenda mbali zaidi na kusema kuwa, ni marufuku kwa Maimamu wa Misikiti kutoa hotuba au kufanya kikao misikiti pasina kupata kibali cha serikali.

Kabla ya hapo pia Wizara ya Masuala ya Kiislamu na Miongozo ya Saudi Arabia ilikuwa imepiga marufuku kufanyika makongamno ya aina yoyote, mikutano, kusambaza na kueneza magazeti na majarida ya kielimu na utoaji miongozo katika shule za nchi hiyo isipokuwa kwa kupata kibali rasmi kutoka kwa Naibu Waziri. Marufuku hiyo dhidi ya raia inatangazwa na viongozi wa ukoo wa Aal Saudi katika hali ambayo, watawala wa nchi hiyo wamekuwa wakitumia suhula zote za nchi zikiwemo fedha za pato la mafuta kwa ajili ya kueneza fikra na mafundisho potofu ya Uwahabi. Katika uga huo, kumefichuliwa ripoti inayoonesha juu ya kutumiwa fedha nyingi mno na watawala wa Saudia kwa ajili ya kueneza fikra za Kiwahabi ambazo ndizo chimbuko la itikadi za kigaidi na kitakfiri. Chris Murphy Seneta wa Kimarekani amefichua katika Baraza la Uhusiano wa Kigeni la Marekani kwamba, Saudia imetumia dola bilioni mia moja kwa ajili ya kueneza fikra na mitazamo ya Kiwahabi. Hatua ya watawala wa Saudia ya kuzidi kubinya anga ya kisiasa, kijamii na kiutamaduni ya Saudia na wakati huo huo kukiuka haki za binadamu ni mambo ambayo yanazidi kuweka wazi mbele ya macho ya walimwengu utambulisho halisi wa utawala huo.

Utawala wa Saudi Arabia ambao umejengeka juu ya misingi ya udikteta umekuwa ukiendesha sera za ukandamizaji na za mkono wa chuma dhidi ya raia na kama ulivyo utawala wowote ule wa kidikteta, nao umekuwa ukitekeleza hayo katika juhudi zake za kuhakikisha unaendelea kubakia madarakani. Takwimu za duru za haki za binadamu zinaonesha kuwa, idadi ya wafungwa nchini Saudia imefikia elfu thelathini, jambo ambalo linaonesha kukita mizizi siasa za kipolisi za utawala wa Aal Saud dhidi ya wananchi wa nchi hiyo. Ukweli wa mambo ni kuwa, mfumo wa utawala wa Aal Saud ni wa kurithishana ambapo wananchi hawana nafasi yoyote ile katika uendeshaji wa masuala ya nchi yao au utungaji sheria. Hakuna hata nembo moja kama kufanyika uchaguzi, kuweko vyama vya kisiasa au uhuru wa magazeti ambayo ipo nchini Saudia inayoonesha kwamba, utawala ulioko madarakani una ridhaa na baraka za wananchi. Katika mazingira kama haya, watawala wa Saudia wameshadidisha ukandamizaji dhidi ya wananchi wanaowakosoa. Ukandamizaji wa viongozi hao unafanyika kwa minajili ya kuzima sauti ya wananchi wa nchi hiyo inayoapazwa kwa ajili ya kutaka uhuru. Pamoja na hayo, kuendelea malalamiko na maandamano ya amani na sisitizo la kuendeleza njia ya baba yake, mtoto wa Sheikh Nimr Baqir al-Nimr mwanazuoni ambaye alinyongwa na utawala wa Saudia kwa sababu tu ya kupigania haki za wananchi, ni jambo linaloonesha juu ya kutokuwa lelemama harakati ya wananchi wa nchi hiyo na kusimama kwao kidete kunathibitisha kwamba, hawatetereshwi na ukandamizaji wa watawala wa ukoo wa Aal Saud.