IOM: Mamia ya wahajiri wamefariki dunia tangu mwanzoni mwa mwaka huu
Shirika la Kimataifa la Wahajiri (IOM) limeripoti kuwa, mamia ya wahajiri wamefariki dunia katika wiki sita tu za mwanzoni mwaka huu wa 2016.
Ripoti iliyotolewa na shirika hilo imesema kuwa, katika wiki sita za mwanzoni mwa mwaka huu wa 2016 wakimbizi wasiopungua 409 wamefariki dunia kwa kughiriki katika bahari ya Mediterania wakiwa mbioni kuelekea Ulaya. Ripoti hiyo inasema idadi hiyo ni mara 10 zaidi ya takwimu za mwaka uliopita.
Ripoti ya shirika la IOM imesema kuwa, tangu tarehe Mosi Januari hadi sasa wakimbizi elfu 76 wameingia Ulaya kiwango ambacho ni sawa na wakimbizi elfu mbili kwa kila siku.
Awali Shirika la Wahajiri la Kimataifa lilitangaza kuwa, wakimbizi zaidi ya milioni moja waliingia barani Ulaya mwaka uliopita na karibu ya wengine 3700 wamefariki dunia baada ya kuzama katika Bahari ya Mediterania.
Idadi kubwa ya wakimbizi hao wanatoka katika ameneo yenye ghasia na machafuko yanayosababishwa na makundi la kigaidi kama lile la Daesh linaloungwa mkono na kusaidiwa kwa hali na mali na nchi kama Marekani, Saudi Arabia, Qatar, Uturuki na waitifaki wao.