Holocaust ya karne mara hii yatekelezwa Gaza
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i103712-holocaust_ya_karne_mara_hii_yatekelezwa_gaza
Wakati dunia ingali katika mshangao wa kushambuliwa kwa mabomu hospitali iliyojaa Wapalestina waliojeruhiwa na jeshi la utawala ghasibu wa Israel, mashambulizi makali ya anga na makombora ya utawala huo yangali yanaendelea dhidi ya Ukanda mzima wa Ghaza kwa wiki ya pili mfululizo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 20, 2023 09:00 UTC
  • Holocaust ya karne mara hii yatekelezwa Gaza

Wakati dunia ingali katika mshangao wa kushambuliwa kwa mabomu hospitali iliyojaa Wapalestina waliojeruhiwa na jeshi la utawala ghasibu wa Israel, mashambulizi makali ya anga na makombora ya utawala huo yangali yanaendelea dhidi ya Ukanda mzima wa Ghaza kwa wiki ya pili mfululizo.

Mashambulizi ya utawala wa Kizayuni katika Hospitali ya al-Maamadani ya Ghaza na mauaji ya kutisha ya wanawake, watoto na wazee yanahesabiwa kuwa jinai kubwa zaidi ya kivita na mauaji ya kimbari katika karne hii.

Wahanga hao aidha walienda hospitali kuwahudumia majeruhi wao, au walidhani kwamba mahali hapo palikuwa salama kutokana na mashambulizi ya utawala wa Kizayuni kwa mujibu wa kanuni za kimataifa.

Kwa mujibu wa uthibitisho wa Wizara ya Afya ya Palestina, wahanga wote wa mashambulizi ya kinyama ya Wazayuni katika Hospitali ya Al-Maamadani katika Ukanda wa Gaza walikuwa raia wa kawaida.

Katika historia, nchi zinazopigana daima zimekuwa zikizingatia viwango vya chini zaidi vya sheria za kimataifa, ikiwa ni pamoja na kulindwa hospitali na vituo vya matibabu dhidi ya mashambulizi, lakini utawala haramu wa Israel hauzingatii sheria zozote za kimatifa, ambapo sasa kufuatia malalamiko makubwa ya jamii ya kimataifa, unafanya juhudi za kufunika jinai hiyo na kujiondolea lawama kuhusiana na shambulio hilo la kinyama dhidi ya watu wasio na hatia.

Inaonekana kwamba Wazayuni wametegemea sana kitabu chao cha Talmud katika kutekeleza jinai za kiholela dhidi ya Wapalestina kwa sababu kwa mujibu wa maandiko ya kitabu hicho, mtu yeyote asiye Myahudi anapasa kuuawa, hata kama atakuwa ni mwema na msafi kiasi gani."

Sehemu ya jinai za Wazayuni dhidi ya Wapalestina

Katika hali ya hivi sasa, kuendelea jinai za kivita za Israel katika mazingira ya upuuzaji wa kimataifa na ushirikiano wa serikali za Magharibi na Tel Aviv, kumekifanya kikao cha dharura cha Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu mjini Jeddah kuwa tumaini la pekee la watu wa Ghaza.

Hata kama sehemu ya jinai za kivita za Israel dhidi ya wakazi wa Ghaza inatokana na ubaguzi wa rangi na siasa za kupindukia mipaka za baraza la mrengo wa kulia la Netanyahu, lakini sehemu nyingine ya jinai hizo inatokana na kutojali mashirika na tasisi za kimataifa na kikanda, na vile vile undumakuwili wa serikali za Magharibi, ambazo hivi karibuni zimetumia veto zao katika Baraza la Usalama kupinga maazimio yaliyokusudia kukomesha jinai za utawala wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina wasio na hatia.

Moja ya sifa za operesheni ya kushangaza ya Kimbuka cha Al-Aqsa ni kwamba mwanzoni iliweza kubadilisha idadi ya Wazayuni waliouawa na kujeruhiwa, kwa maslahi ya Wapalestina. Hivyo, moja ya malengo ya utawala wa Kizayuni tangu mwanzo limekuwa ni kubadilisha hali hiyo na kusababisha vifo na majeruhi wengi zaidi kati ya Wapalestina kiasi cha kujiweka katika mazingira mazuri zaidi katika uwanja huo.

Ijapokuwa idadi ya wahanga wa Palestina hivi sasa imepindukia mara kadhaa ile ya Wazayuni, lakini bado utawala huo wa kibaguzi na waungaji mkono wake wa Magharibi hawaridhishwi na suala hilo, hivyo wanaendelea kuwachinja Wapalestina bila huruma.

Katika siku chache zilizopita, utawala wa Kizayuni umewataka wakazi zaidi ya milioni moja wa eneo la kaskazini mwa Ukanda wa Gaza kuondoka katika eneo hilo ili kuandaa mazingira ya kuanza operesheni za nchi kavu katika ukanda huo, lakini kwa vile wakaazi wa Ghaza wanapinga kuondoka katika eneo hilo, nayo Misri haiwakubalii kuingia katika ardhi yake, utawala wa kigaidi wa Israel umeamua kushambulia hospitali ya Al-Maamadani kwa shabaha ya kuwalazimisha wakazi hao wa Gaza kuondoka huko.

Takwimu zinaonyesha kuwa zaidi ya Wapalestina 3,000 wameuawa shahidi na wengine 12,000 wamejeruhiwa kutokana na mashambulizi ya mabomu ya utawala wa Kizayuni ambapo nusu yao ni wanawake na watoto.

Wakati huo huo, kwa mujibu wa mkurugenzi wa mawasiliano wa UNRWA, Wapalestina milioni moja wamekimbia makazi yao huko Gaza tangu kuanza vita vya Oktoba 7.

Ili kuzuia kuakisiwa jinai zake huko Ghaza, ambazo baadaye zinaweza kutumika kama hoja ya kufuatiliwa na kushtakiwa wanajeshi na maafisa wa kisiasa wa utawala wa Israel, hususan wanachama wa Baraza la Mawaziri la Netanyahu lenye misimamo ya kupindukia mipaka, utawala wa Kizayuni unalenga kwa makusudi waandishi wa habari, na matokeo yake ni kuuawa zaidi ya waandishi 18 wa vyombo vya habari.

Unyama wa Wazayuni dhidi ya Wapalestina

Kadhalika, ili kusababisha majeruhi zaidi miongoni mwa raia wa Palestina, baraza la mawaziri la Netanyahu linatumia mabomu mazito na yaliyoharamishwa dhidi yao na  pia kulenga kwa makusudi wafanyakazi wa mashirika ya misaada ya kibinadamu na kuzuia kuingia midaa ya dharura ya madawa na chakula ndani ya Gaza.

Kwa mujibu wa Mkataba wa Roma, makosa manne au jinai za kimataifa ni miongoni mwa uhalifu unaopasa kushughulikiwa na Majakama ya Kimataifa ya Jinai ICC, ambao ni pamoja na mauaji ya halaiki, uhalifu wa kivita, jinai dhidi ya binadamu na jinai ya ubakaji.

Jinai zote hizo zimetekelezwa na utawala wa Kizayuni huko Ghaza katika siku 14 zilizopita.

Nchi za Kiislamu zinaweza kuunda mahakama maalumu ya kushughulikia jinai za utawala wa Kizayuni ili kuufanya usithubutu tena kutenda jinai hizo za wazi dhidi ya Wapalestina.

Kuwatimua mabalozi wa utawala wa Kizayuni katika nchi za Kiislamu na Kiarabu na kususia ununuzi wa bidhaa za Marekani na Israel na nchi nyingine za Magharibi ambazo zinaunga mkono jinai za utawal huo huko Ghaza ni njia nyingine muwafaka ya kukabiliana na Wazayuni watendajinai.