Hatimaye Netanyahu amdhibiti Biden
(last modified Sat, 21 Oct 2023 02:24:25 GMT )
Oct 21, 2023 02:24 UTC
  • Hatimaye Netanyahu amdhibiti Biden

Biden ambaye awali alijiepusha kumwalika Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala wa kibaguzi wa Israel katika Ikulu ya White House, ameshawishika kukubali hila za Netanyahu, ambapo amesimamisha shughuli zake zote huko Marekani na kuamua kumtembelea katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu katika kilele cha uzee wake.

Safari hiyo imefanyika wakati Israel ikitumia bomu la tani moja la Marekani imewaua raia waliokimbilia katika hospitali ya Al-Maamadani, ambao waliamini kwamba wangesalimika kutokana na mashambulizi ya anga ya utawala huo na hiyo ni baada ya Tel Aviv kutoa dhamana ya kuwa kwao salama katika maeneo hayo. Aidha, kwa mujibu wa sheria za kimataifa, mashambulizi dhidi ya raia na vituo vya kiraia kama vile hospitali yanachukuliwa kuwa jinai za kivita.

Hata hivyo, kwa vile jinai za kivita za Israel hazichukuliwi hatua za kisheria kutokana na misimamo ya undumakuwili inayotawala katika anga ya kimataifa na pia uungaji mkono wa serikali za Magharibi hususan Marekani, utawala huo huendeleza jinai zake kwa kujiamini kabisa kuwa hautachukulia hatua yoyote ya kisheria na jamii ya kimataifa na kwa mtazamo huo, serikali za Magharibi na taasisi za kisiasa na kiusalama za Kimataifa kama vile Baraza la Haki za Binadamu na vilevile Mahakama ya Kimataifa ya Jinai zinabeba sehemu ya dhima ya jinai za utawala huo wa Kizayuni.

Wanga wa mashambulizi ya Ghaza

Kuhusiana na suala hilo, ingawa katika siku 14 zilizopita, baada ya kuanza duru mpya ya mashambulizi ya utawala wa Kizayuni huko Ghaza, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilifanya vikao viwili, lakini vikao hivyo vilimalizika bila natija yoyote ya maana kutokana na kura ya turufu ya Marekani. Hii ni katika hali ambayo maazimio yaliyopendekezwa katika vikao hivyo yalikuwa ya kibinadamu kabisa kutokana na ukweli kwamba yalisisitiza kuzingatiwa kanuni na sheria za kimataifa pamoja na haja ya kuwasaidia wakazi wa Ukanda wa Ghaza walio chini ya mzingiro wa Israel.

Awali, ilidhaniwa kuwa  kura ya turufu  ya azimio la kwanza  ni kutokana na kuwa iliwasilishwa na Russia, lakini kura ya turufu ya azimio lililopendekezwa na Brazil ilionyesha kuwa serikali za Magharibi, hasa Marekani na Rais Biden mwenyewe, wanacheza mchezo  mmoja na Netanyahu ambaye anafanya kila awezalo hata kama ni kutekeleza jinai za kivita, ili kufunika siasa zake za ndani, kama vile kufedheheshwa kijeshi katika kukabiliana na operesheni ya Kibunga cha al-Aqsa au kuunda umoja bandia wa ndani ili kudhibiti migawanyiko ya ndani, na anaendeleza  mauaji ya kimabari ya makusudi na kuwalazimisha kuhama zaidi ya wakazi milioni mbili wa Ukanda wa Ghaza.

Rais Biden (kulia) na Netanyahu

Wakati huo huo, safari ya Biden katika Palestina inayokaliwa kwa mabavu katikati ya mauaji kizazi ya wakazi wa Ghaza, hasa watoto na wanawake, sio tu kwamba inaifanya Marekani kuwa mshirika wa Netanyahu mauaji hayo, kwa sababu yamefanywa na ndege za Kimarekani aina ya F-16 na mabomu yake ya tani moja, bali inauhimiza pia utawala huo kuendelea na jinai hizo na kufanya mashambulizi ya nchi kavu kwa ajili ya kuiangamiza kabisa Ghaza. Kwa mtazamo huo, inaonekana kuwa matokeo ya safari ya Biden huko Israel  ni kuendelezwa mashambulizi makali ya kinyama na kigaidi ya utawala wa Kizayuni dhidi ya wakazi wa Ukanda wa Ghaza.