Nafasi muhimu ya Ansarullah katika kusitishwa vita na kuendelea kwake
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i105360-nafasi_muhimu_ya_ansarullah_katika_kusitishwa_vita_na_kuendelea_kwake
Naibu Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa serikali ya muda ya Yemen yenye mfungamano na Harakati ya Ansarullah amesema, tunakumbusha kwa mara nyingine tena kwamba, usafiri wa meli utakuwa salama kwa meli zote isipokuwa meli za utawala wa Israel katika Bahari Nyekundu.
(last modified 2023-11-28T23:13:17+00:00 )
Nov 28, 2023 23:13 UTC
  • Nafasi muhimu ya Ansarullah katika kusitishwa vita na kuendelea kwake

Naibu Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa serikali ya muda ya Yemen yenye mfungamano na Harakati ya Ansarullah amesema, tunakumbusha kwa mara nyingine tena kwamba, usafiri wa meli utakuwa salama kwa meli zote isipokuwa meli za utawala wa Israel katika Bahari Nyekundu.

Hussein Al-Azzi ameandika ujumbe kwenye mtandao wa kijamii wa X: "Bila shaka, Sana'a inavutiwa zaidi na usalama wa meli na inaheshimu maslahi ya ulimwengu zaidi ya yote. Haya ndiyo tuliyothibitisha huko nyuma. Tunasisitiza tena ya kwamba: Usafiri wa meli utakuwa salama kwa meli zote isipokuwa meli za utawala wa Israel katika Bahari Nyekundu hadi utawala huo ghasibu utakapokomesha uvamizi wake dhidi ya watoto na raia wasio na ulinzi katika Gaza inayodhulumiwa."

Hii ni radiamali ya kwanza ambayo Harakati ya Ansarullah kwa ripoti kuhusu kutekwa nyara meli ya Israel na vikosi vya ulinzi katika eneo mkabala na Aden kusini mwa Yemen.

Mbali na mashambulizi ya makombora na ndege zisizo na rubani katika maeneo ya Palestina yanayokaliwa kwa mabavu, Ansarullah inatekeleza stratejia na mkakati mpya kwa ajili ya kukabiliana na adui Mzayuni.

Yahya Saree, msemaji wa jeshi la Yemen

 

Msemaji wa jeshi la Yemen ametangaza kuwa, kwa mujibu wa dhima ya kidini, kitaifa na kimaadili na kwa kutilia maanani hujuma za kila siku za utawala wa Kizayuni na Marekani katika Ukanda wa Gaza na mauaji ya wananchi wa Palestina, na kwa ajili ya kukidhi matakwa. ya taifa la Yemeni na mataifa yote huru ya dunia, meli yoyote ambayo ina sifa zifuatazo italengwa:

1.      Meli ambazo zinapeperusha bendera ya utawala wa Kizayuni wa Israel.

2.      Meli zinazoendeswa na mashirikka ya Israel.

3.      Meli ambazo zinamilikiwa na mashirikka ya Israel.

Jeshi la Yemen pia limezitaka nchi zote za dunia kuwaondoa raia wao wanaofanya kazi ya kuhudumu kwenye meli hizo, kuacha kushirikiana na meli za Israel katika kupakia na kupakua mizigo na kuzijulisha meli zao kuwa mbali na meli za Israel.

Masiku haya tuliyonayo yanashuhudia usitishaji vita wa muda huko Gaza na Bahari Nyekundu imegeuka na kuwa kambi kuu ya kukabiliana makundi ya muqawama dhidi ya utawala wa Kizayuni, na katika hatua ya hivi karibuni ya Ansarullah ya Yemen ya kuwaunga mkono watu wa Gaza, ni ya kuiteka meli ya tatu ya utawala wa Kizayuni.

Baada ya kukamata meli mbili za kibiashara za Israel wiki iliyopita, Wayemen waliiteka meli ya tatu ya Israel siku ya Jumapili. Habari za kukamatwa kwa meli ya tatu ya Israel katika pwani ya Yemen ni mshtuko mwingine uliowapata Wazayuni jana na kuongeza zaidi machungu ya kushindwa hivi karibuni na muqawama hukio Palestina. Hii ni kwa sababu, mgogoro wa kukamata meli za Israel utateteresha kivitendo uchumi unaoyumba wa utawala wa Kizayuni.

Kusimamisha harakati za meli za kibiashara na zisizo za kibiashara za utawala unaoikalia kwa mabavu Quds katika Bahari Nyekundu kumeufanya uchumi wa utawala huo wa Kizayuni kuwa katika mgogoro zaidi kuliko hapo awali.

 

Meli za kibiashara zilizokuwa zimebeba mizigo kutoka kwa makampuni ya Israel zilisimamisha safari zao kabla ya kufika Bab al-Mandab na kurudi kwenye bandari zilizotoka.

Meli ambazo zilitakiwa kubeba mizigo mbalimbali ya kibiashara kwa ajili ya kuingizwa Israel kutoka bandari za nchi za Asia zikiwemo meli za mizigo, vyakula na vifaa vya ujenzi bado hazijaondoka.

Tukiangazia gharama za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja za vita vya utawala wa Kizayuni dhidi ya Gaza kufuatia operesheni ya kimbunga ya Al-Aqsa tunaona kuwa, hali ya kiuchumi haiwaruhusu viongozi wa utawala unaoukalia kwa mabavu Quds kuendelea na vita bila ya kikomo cha muda.

Bahari Nyekundu, na hasa Lango Bahari la Bab al-Mandab, ndio ukanda wa baharini muhimu zaidi na uti wa mgongo wa uchumi wa Israel, unaounganisha korido ya Bahari ya Hindi na maeneo yanayokaliwa kwa mabavu, na kuhatarisha mshipa huu mkuu kunaweza kusababisha hasara isiyoweza kufidika kwa uchumi wa utawala huu.

Giora Eiland, Mkuu wa zamani wa Baraza la Usalama wa Ndani la utawala wa Kizayuni alisema Jumapili iliyopita kwamba, Yemen ni tishio la kistratijia kwa Israel. Katika taarifa yake katika Kanali 12 ya Televisheni ya Kizayuni, Eiland alisema: "Tatizo letu na Wayemen linahusiana na nafasi yao ya kijiografia katika Lango Bahari la Bahari Nyekundu na sehemu yake ya kusini, na tatizo hili ni zaidi ya suala la makombora katika nchi hii." "Tatizo kubwa litakuja pale Wayemeni watakapotaka kukamata kila meli ya Israel, kwa hivyo ni jinsi gani usafiri wa baharini unaweza kutolewa kwa bandari ya Eilat."

 

 

Tangu kuanza mashambulizi ya utawala wa Kizayuni katika eneo la Ukanda wa Gaza, utawala wa Kizayuni umekuwa ukiishi katika jinamizi la kufunguliwa mapambano ya muqawama katika eneo hilo, lakini jinamizi hilo hivi sasa limetokea katika ulimwengu wa kweli na hakuna sehemu yoyote katika eneo hilo ambayo ni salama kwa wavamizi.

Kwa kuzingatia kwamba mamlaka za Kizayuni zimetishia kuanzisha tena mashambulizi yao baada ya kumalizika kwa usitishaji vita huko Gaza, katika kadhia hii huenda meli nyingi zaidi zitawindwa. Kwa kuzingatia hilo, inaweza kusemwa kuwa, kama ambavyo kwa kuingia katika vita vya Gaza, Harakati ya Asarullah iliulazimisha utawala wa Kizayuni kukubali usitishaji vita, vivyo hivyo itakuwa na nafasi muhimu katika kuendelea kwa vita hivyo.