Wazayuni wakiri kushindwa katika vita vya Gaza
(last modified Thu, 28 Dec 2023 04:21:54 GMT )
Dec 28, 2023 04:21 UTC
  • Wazayuni  wakiri kushindwa katika vita vya Gaza

kuchukua muda mrefu vita vya Gaza kumewafanya, baadhi ya Wazayuni kukiri kushindwa utawala ghasibu wa Israel katika vita vyake vya jinai huko Gaza.

Dan Halots, mkuu wa zamani wa jeshi la Israel, amesema kwamba Wazayuni wameshindwa vita na mafanikio na ushindi pekee ambao unaweza kupatikana kutokana na vita hivyo ni kujiondoa Benjamin Netanyahu madarakani. Avor Shalah mkuu wa kamati ya mambo ya nje na usalama katika duru iliyopita ya bunge la Kizayuni, pia amekiri kuwa Israel haina uwezo wa kuiangamiza Hamas.

Lakini swali muhimu ni kuwa je, ni dalili zipi zinazoonyesha kushindwa utawala wa Kizayuni katika vita vya Gaza?

Ishara ya kwanza ni kuchukua muda mrefu vita hivyo. Hadi sasa, siku 82 zimepita tokea vita vilipoanza na  haijulikani vitadumu kwa muda gani. Baada ya Intifadha ya pili, mapigano ya utawala wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina yaliyochukua muda mrefu yalikuwa ni ya siku 51, ambayo yalijiri mwaka 2014. Kurefuka vita vya hivi sasa kumekuja katika hali ambayo mapigano hayo hayana uwiano wa nguvu yaani utawala wa Kizayuni una zana na nguvu kubwa zaidi ya kijeshi ukilinganishwa na Hamas. Pamoja na hayo lakini hadi sasa, baada ya kupita siku 82 za vita, utawala huo wa Kizayuni bado haujafikia malengo yake ya kijeshi.

Kujeruhiwa askari vamizi

Dalili ya pili ni idadi ya wanajeshi wa utawala wa Kizayuni walioangamizwa, kujeruhiwa au wasiojulikana waliko. Kwa mujibu wa Dan Halots, mkuu wa zamani wa jeshi la Israeli, hadi sasa zaidi ya askari jeshi 1,300 wameangamia na 2,400 kutekwa nyara. Kwa mujibu wa Halots, hadi sasa kuna zaidi ya watu 1,300 waliouawa na 2,400 waliotekwa nyara, na baadhi yao wameachaliwa huru. Mbali na hayo, hatupaswi kusahau kwamba ndani ya Israeli kuna zaidi ya wakimbizi 200,000 waliolazimika kuhama makazi yao. Anasema kwa kuzingatia hali hiyo, ushindi pekee unaoweza kupatikana ni kumuondoa waziri mkuu madarakani.

Dalili ya tatu ni kushindwa utawala wa Kizayuni kufikia lengo lake la kuiangamiza Hamas. Mwanzoni mwa vita, utawala wa Kizayuni ulitangaza rasmi kuiangamiza Hamas kuwa moja ya malengo yake makuu. Hata hivyo, sio tu kwamba Hamas haijaangamizwa, bali Wazayuni wenyewe wanakiri kwamba Hamas haiwezi kuangamizwa. Ishaq Brik, Meja jenerali wa jeshi la akiba wa utawala wa Kizayuni pamoja na kusifu uwezo wa mahandaki ya Hamas amesema: Msiyaamini maneno ya jeshi na wachambuzi wa Israel. Hakuna uwezekano wa kuyaaribu mahandaki ya Hamas. Idadi ya wanamapambano wa Hamas waliouawa ni ndogo sana. Ishaq Brik ameendelea kusema: Kuharibu mashimo na mahandaki ya Hamas kutachukua miaka mingi na kusababisha vifo zaidi vya askari wa Waisraeli. Makamanda wanaopigana Gaza wanasema hakuna kizingiti cha kuizuia Hamas isikarabati vikosi vyake.

Kukiri Jenerali wa Kizayuni kupoteza wanajeshi wake

Dalili ya nne ya kushindwa utawala wa Kizayuni katika vita vya Gaza ni kushadidi mvutano ndani ya ardhi zinazokaliwa kwa mabavu. Baadhi ya Wazayuni wanaonya kwamba hitilafu hizo za ndani zinaweza hata kusababisha migogoro mikubwa ya ndani katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu. Dan Halots, mkuu wa zamani wa jeshi la Israeli, ameonya kuhusiana na suala hilo na kusema Israeli iko katika hatari ya kuingia kwenye vita vya mitaani, ambapo upande mmoja utakuwa ni wa wanamgambo wa Ben Gvir, Waziri wa Usalama wa Ndani wa utawala wa Kizayuni.

Kukiri wazi baadhi ya Wazayuni kuhusu kushindwa jeshi la utawala ghasibu wa Kizayuni katika kukabiliana na Wapalestina na hasa wapiganaji wa Hamas, kunaonyesha wazi kuwa hata mabadiliko ya madaraka katika Palestina inayokaliwa kwa mabavu yatakuwa kwa manufaa ya Wapalestina, na kuwa kuanzia sasa Israel inapsa kutazama upya sera zake.