Waandamanaji wachoma moto ubalozi mdogo wa Israel mjini Istanbul
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i112288-waandamanaji_wachoma_moto_ubalozi_mdogo_wa_israel_mjini_istanbul
Ubalozi mdogo wa utawala wa Kizayuni wa Israel mjini Istanbul Uturuki umechomwa moto na waandamanaji wenye hasira waliokuwa wakilalamikia vita na mauaji yanayofanywa na utawala haramu wa Israel dhidi ya wananchi wa Palestina katika ukanda wa Gaza.
(last modified 2024-05-28T07:12:55+00:00 )
May 28, 2024 07:12 UTC
  • Waandamanaji wachoma moto ubalozi mdogo wa Israel mjini Istanbul

Ubalozi mdogo wa utawala wa Kizayuni wa Israel mjini Istanbul Uturuki umechomwa moto na waandamanaji wenye hasira waliokuwa wakilalamikia vita na mauaji yanayofanywa na utawala haramu wa Israel dhidi ya wananchi wa Palestina katika ukanda wa Gaza.

Maelfu ya watu wanaripotiwa kuandamana mjinii Istanbul nchini Uturuki na kukusanyiika mbele ya ubalozi mdogo wa Israel kabla ya kuchukua hatua ya kuchoma jumba la ubalozi huo mdogo.

Katika jinai yake ya hivi karibuni zaidi, jeshi la utawala ghasibu wa Israel lilishambulia kwa makombora 7 mahema na kambi za wakimbizi katika eneo la kaskazini-magharibi mwa mji wa Rafah na matokeo yake Wapalestina wasiopungua 41 waliuawa shahidi na makumi ya wengine kujeruhiwa.

Ofisi ya habari ya serikali ya Palestina katika Ukanda wa Gaza imetangaza kuwa, jeshi la utawala ghasibu wa Israel katika kipindi cha masaa 24 yaliyopita limeshambulia maeneo ya makazi ya wakimbizi wa Kipalestina zaidi ya 10 huko Rafah na kuwauwa shahidi zaidi ya Wapalestina 190. 

Wakati huo huo jinai za utawala ghasibu wa Israel katika mji wa Rafah zimeendelea kulaaniwa kila kona duniani.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeitisha kikao kwa ajili ya kujadili jinai hizo za Israel.

Hata hivyo, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa nalo limeendelea kukosolewa kutokana na kushiindwa hadi sasa kuchukua hatua za maana za kukomesha jinai hizo za Israel.