Ujumbe wa Umoja wa Mataifa kuondoka Iraq mwishoni mwa mwaka ujao
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limjepasisha kwa pamoja uamuzi wea kuondoka Iraq ujumbe ujumbe wa kisiasa wa umoja huo.
Ripoti zinaeleza, kwa mujibu wa uamuzi wa Baraza la Usalama ujumbe huo utaondoka nchini nchini Iraq mwishoni mwa mwaka ujao wa 2025 baada ya kuweko huko kwa zaidi ya miaka 20.
Uamuzi huo umechukuliwa baada ya Umoja wa Mataifa kupokea ombi la serikali ya Iraq la kumaliza kazi za ujumbe huo.
Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa lilipasisha uamuzi huo hapo baada ya kuongeza muda wa ujumbe huo hadi tarehe 31 Desemba mwaka 2025 ambapo UNAMI itasitisha kazi zake zote katika nchi hiyo ya Kiarabu.
Kwa upande wake serikali ya Iraq imekaribisha uamuzi huo ikisema unaashiria maendeleo na uthabiti uliopo nchini humo tangu ujumbe huo wa Umoja wa Mataifa wa usaidizi wa Iraq UNAMI ulipoundwa mwaka 2003, baada ya uvamizi ulioongozwa na Marekani kwa ajili ya kuuangusha utawala wa dikteta Sadam.
Ujumbe huo una wafanyakazi takriban 700 ambao kazi yake ni kuishauri serikali kuhusu mazungumzo ya kisiasa na maridhiano pamoja na kusaidia katika masuala ya uchaguzi na mageuzi ya kiusalama.